Tunduru Korosho FC yapoke Basi kutoka Japan

Tunduru Korosho FC yapoke Basi kutoka Japan

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katika kujiimarisha kuelekea kwenye michuano ya NANE BORA (TOP 8) ya Ligi Daraja la Pili (First League - FL) itakayofanyikia jijini Mwanza kuanzia tarehe 15 Aprili 2022, Timu ya Tunduru Korosho FC maarufu kama Watoto wa Wakulima wa Korosho imepokea basi jipya aina ya Toyota Coaster lenye uwezo wa kubeba watu 30 kutoka nchini Japan.

Basi hilo lililonunuliwa kwa juhudi za wadau wa maendeleo ya Tunduru waliounganishwa na Julius Mtatiro Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, limepokelewa leo mjini Tunduru na mamia ya mashabiki wa timu hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro ameeleza timu ya Tunduru Korosho inapiganiwa vilivyo ili ipande daraja na kwenda Ligi ya Championship msimu ujao, amewataka viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kuiunga mkono ili kuitangaza wilaya ya Tunduru, mkoa wa Ruvuma na zao la korosho.

Akiwasilisha ripoti ya ununuzi wa basi hilo, Katibu wa Tunduru Korosho FC Kaitara Bwire alisema ununuzi wa basi, kulisafirisha kutoka Japan, kulilipia ushuru na masuala yote muhimu vimegharimu shilingi Milioni 55.4 huku akiwasilisha nyaraka zote za manunuzi hadi kuitoa bandarini Dar Es Salaam, ikiwa ni pamoja na kukabidhi kadi halisi ya gari hilo kwa Mkuu wa Wilaya.

Mtatiro amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea na wajibu wake wa kusimamia sekta zote muhimu za maisha ya mtanzania ikiwemo sekta ya michezo na kuahidi kuendelea kusimamia mambo makubwa kimichezo katika wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa Tunduru Korosho FC Mohamed Kiyonjo ameshukuru juhudi za wadau na mikakati ya Mkuu wa Wilaya katika kuendeleza michezo wilayani humo na amewataka wasirudi nyuma.

Bwana Musa Manjaule, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU) ameeleza TAMCU na wadau wengine wa mazao wilayani Tunduru walishaamua na wataendelea kuwa sehemu ya juhudi za kufufua na kuendeleza michezo wilayani Tunduru ikiwemo kuisaidia timu ya Tunduru Korosho.

Imeandaliwa na;

Ismail Said,
Afisa Habari TKFC,
Tunduru - Ruvuma
31 Machi 2022

IMG-20220331-WA0014(1).jpg


IMG-20220331-WA0004.jpg


IMG-20220331-WA0014.jpg


IMG-20220331-WA0012.jpg


IMG-20220331-WA0010.jpg
 
Sio mbaya mwanzo mzuri Sana

Azam timu kubwa walinunua basmwez mzma.likiwa safarin hatujalala Kila siku tunaambiwa lipo njian

Tunduru mmenunua bas bila kelele haijalishi bas gan bas n bas TU

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom