Hofu imetanda katika wilaya ya Tunduru , kutokana na Mauaji na kutekwa kwa vijana waendesha boda boda.
Taarifa kutoka mjini Tunduru zinasema , vijana wa bodaboda wamekuwa wakipotea baada ya kukodiwa na watu, wanaojifanya wanakwenda vijiji vya mbali na Tunduru.
Katika tukio la hivi karibuni kijana mmoja alikodiwa na watu wasiojulikana tarehe 12/8/2022.Na baadae mwili wake ulikuja kuonekana maeneo yanayoitwa Nandembo ,akiwa amefariki.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, vijana kadhaa wameshapotea katikati ya mwezi wa saba na nane mwaka huu na bado hawajaonekana. Vitendo hivyo vya kikatili kwa vijana hao wadogo waendesha bodaboda vinahusishwa na wizi wa bodaboda hizo ,ambazo inasemekana zimekuwa na soko kubwa katika nchi ya jirani ya Msumbiji. Wauaji hao, Mara baada ya Mauaji hayo uondoka na boda hizo na kuzipeleka huko Msumbiji ambako Kuna soko kubwa. Pia kumekuwa na taarifa kwamba boda hizo hutumiwa kutengeneza injini ya boti katika nchi hiyo.
Wakazi wa wilaya hiyo wamemuomba mkuu wa wilaya na jeshi la polisi kuchukua hatua kali za kuzuia Mauaji hayo au waagize jeshi la polisi kutoka makao makuu ili waje kufanya uchunguzi .