Azimio la Arusha liliposhindwa ilikuwa ni kwa sababu ya SAP.Hivi China ni nchi ya kijamaa au ni taifa lenye chama kimoja tu kinachoendesha nchi kitemi.
Hakuna mtu aliyemuwekea kamba shingoni mwenzake kwamba ikubali SAP.Ukweli ni kwamba ni uzembe wa Nyerere kushindwa kujua maigizo ya siasa za kidunia ndio anguko letu.Kwani sisi si ndo wale tunadai tulipambania uhuru wetu 1961.Kama ndio, huo uhuru ulikuwa ukimanisha nini na SAP inakuwaje iwe shida kwa watu walio huru?Anyway,hakuna chochote cha maana tulifanya ata huo uhuru ni chenga tu hakuna cha Bibi Titi wala Mwalimu, ni muda tu ulikuwa upande wetu na mahesabu mabovu ya wakoloni basi.
No nyerere hakutaka kukubaliana na mpango wa Structural Adjustment Program (SAP),shida ni kuwa baada ya vita vya nduli, nchi ilifulia kwerikweri,,, [emoji134][emoji134] kipindi hicho kighoma malima ndo waziri wa fedha,, Nyerere na malima hawakutaka kukubaliana na IMF,, so wazungu wakabana kutoa fedha,
Mambo yakawa magumu kwelikweli,, njaa, ukosefu wa ajira, madawa, etc
Nyerere akagoma,,, [emoji23][emoji23]
Hali ikakaza zaidi, ikafuata na njaa ya 1984,, Nyerere amekaza tu, duh,, hatimae akang'atuka asee,
Ruksa alikuta hali mbaya kwerikweri,,, [emoji134][emoji134],hakuwa na jinsi akakubalianana mpango wa SAP.
Yaani structure ya uchumi ibadilishwe, pawepo na uchumi huru, Private sectors iruhusiwe, pawepo na cost sharing katika huduma za elimu, mashule, watu wajiajiri, waanzishe makampuni, viwanda serikali ijitoe katika kufanya biashara, ibaki kukusanya kodi, etc.
Baada ya hapo ukafuata mpango wa kufufua uchumi National Economy Recovering Programme,,
Ambayo mashariti ya kufanya biashara yakarahisishwa, mipaka ikafunguliwa,, haikuwa kosa tena kukutwa na sabuni ya Emperial, kwanga wala Rexona,
Mtu yeyote aliruhueiwa kuagiza vyombo vya usafiri, Tv, etc[emoji23][emoji23][emoji23]