Tungekomaa na Ujamaa bila kuikumbatia SAP labda sasa hivi tungekuwa mbali

kudos
 
Sio kweli mkuu
 
Ujamaa haujawahi fanikiwa popote duniani, ujamaa ni mfumo wa utawala na sio mfumo wa uchumi, kwenye uchumi umefeli.
Lengo kuu la ujamaa ni kutawala watu kwa maslai binafsi ya mtawala au kikundi cha walamba asali wachache katika jamii.
Ujamaa unalenga kumiliki akili za watu kupitia uchumi kwa maana mtu binafsi asimiliki mali kuzidi anaemtawala Ili iwe rahisi kumtawala.
Mwanadamu hawezi kuwa mjamaa ni hadi aushinde ubinafsi. Jamii ikiweza kuushinda ubinafsi ujamaa utawezekana.
Ubinafsi na shauku ya kutaka zaidi uchochea maendeleo.
 
Hakuna sehemu yeyeto Mwalimu alichochea uchumi bali alitumia hazina mali na pesa alizoachiwa na mkoloni ambazo nazo alizitapanya kwenye ukombozi wa nchi za afrika pamoja na vita vya Uganda Ili amrudishe madarakani swahiba wake Obote, kumbuka Mwalimu na Amini zilikuwa haziivi, akamtengeneza propaganda Amin ikiwemo ya uvamizi kagera Ili apate sababu ya kumrejesha madarakani Obote.
 
Ujamaa ni ushetani.
 
Nchi itaendelea iwapo watu watajitolea kwa ajili ya nchi. Shida yetu kubwa ni matangazo ya tutafanya hivi au tunategemea kufanya hivi. Lakini pia ni ile false consciouness tuliyo nayo kwamba bila msaada hatuendi na bila kuwa na wa kufikiri kwa ajili yetu hatuwezi kupiga hatua. Ubungo farm implements tuliua bila kufikiria. Kwa maisha ya kipindi kile tungetumia products za UFI kwenye kilimo leo tungekuwa na kiwanda cha ku assemble matrekta kama si kuunda! Mpaka leo hatujui tunataka nini hasa. Fine, tuliuacha ujamaa je tumefaidika na nini? Kuna haja ya kutakari kama nchi na kuamua mwelekeo sahihi. Tunata kukimbia bila hata kutambaa japo kwa wiki moja?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…