Hivi nikuulize,unadhani Mbowe na Lissu wanashindwa na vishilingi laki3toka kwenye mikutano ya hadhara?umesema inaniasidia nini nawe nikuulize uonapo ripoti ya cag inaonesha rosario itakaa kimya kwakuwa haikuhusu?
Wangekuwa hawashindwi na hizo laki 3 unazosema, wasingetumia mikutano yao kuwachangisha wananchi masikini.
Cha kushangaza wao wanatumia ujinga wa wananchi masikini wanaowaamini kuwachangisha na baadae hela hizo kwenda kula na familia zao huko Ulaya bila kuleta mrejesho wa matumizi ya hela za michango walizochangisha mikutanoni kwako.
Ningewaona wa maana na ningewasifia kama wangekuwa wanatumia pesa hizo kutatua kero za wananchi husika. Mfano wakute sehemu kuna shida ya barabara, au hospital, alaf wachangishe fedha hizo, pamoja na wao kina Mbowe wachangie kwa ajili ya ujenzi wa hospital au barabara ya eneo husika.
Hapo nina imani wananchi watakuwa na Imani nao na watawachagua ktk uchaguzi wowote. Ila swala la kusema eti Lisu tajiri huku haachi mchango hata wa shilingi 100 ya mwananchi masikini, ni kujaribu kutushikia akili watu wenye akili kitu ambacho kamwe hakiwezekani.
Hata huyo Zito kwa vile ni mwanasiasa, basi na yeye ni miongoni mwa wachumia tumbo wakubwa wa nchi hii.
Kuhusu swala la cag kwa vile la kitaifa na lina manufaa kwangu na familia yangu kwa sababu ya kodi yangu, ni lazima nitalisemea.
Sasa wewe kuongelea mambo ya vyama huku wanaokula pesa za vyama ni wakubwa wa vyama na familia zao, hapo lazima nikushangae maana unajipendekeza kwa wasiokujua, na wala watoto wao huko Ulaya wala hawana habari kama wewe unajipendekeza kwenye vyama vya baba zao.