Tunza siri za faragha yako na mpenzi wako usije ukaibiwa

Tunza siri za faragha yako na mpenzi wako usije ukaibiwa

Baba Kisarii

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2024
Posts
1,844
Reaction score
3,089
Hii inahusu wanaume japo yaweza kuwahusu na wanawake pia.

Usifanye huu ujinga baada ya kuonja utamu na mpezi wako - amekupa utamu faragha mkiwa wawili tu yaani wewe na yeye, kisha ukamgeuka na kwenda kuwasimulia watu wako wa karibu, mabest zako, ndugu wa udugu, na washirika wengine wa kiume na marafiki kuhusu "utamu wake ulivyo."

Kiukweli kuna wanawake wengine huwa hawajali watu wengine wanafikiria nini kuhusu utamu wao kusimuliwa kwa mabest lakini huwa na maamuzi ya kuumiza sana kwa mropokaji wakigundua ujinga wake - ukianza kuropoka hawatajali kwa wewe kuwa na domo kubwa la kuwasimulia marafiki zako mnachofanyaga faragha ila watafanya maamuzi.

Kitakachokutokea ni hiki.. "mpenzi wako atakata mawasiliano na wewe hatakupa tena utamu na atakutupa kimya kimya".

Baada ya siku chache utagundua mmoja wa mabest uliyemsimulia kuhusu utamu wa mpenzio kamchukua mpenzi wako na anaishi naye mjengoni kama mke wake mpendwa.

Hapo huhitaji kutafuta mchawi, aliyesababisha hayo yote ni wewe mwenyewe na udomo kaya wako.

Nikuambie tu tuliza jazba kisha ujifunze kuchunga domo lako ili usipoteze tena utakayempata baada ya kuporwa yule wa kwanza.
 
Mwanaume gani anasimulia hayo mambo ya mpenzi wake sasa, nasikiaga wanawake ndo wenye hizo tabia huko masaluni
 
Back
Top Bottom