Tunzi

Tunzi

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Yapata saa tisa za usiku.. alionekana pale,mwenye taharuki..
sura yake dhahiri ilijazwa na hofu,hofu yenye ambato la kutokujua afanye nini!

halikuwa moja lenye kumchanganya, yalikuwa mia! alitaharuki tena baada ya kusikia ngurumo ya radi.. alitamani kulia lkn chozi halikuwa rafiki naye.. upepo wenye kutisha ulivuma,mtoto wake pia aliendelea kung'aka
kijasho kizito kilimtoka kwa pupa!

Alikuwa ni binti wa miaka 19 tu,uzuri wake ulifufishwa kwa majukumu ya ukubwani!
ni miezi mitano tu toka ajifungue mtoto wake wa kwanza,aliempachika jina la Aduhule!..

Alitazama kibanda chao cha nyasi na tope,tumaini la kupona lilipeperuka moyoni mwake!.. aliuona mwisho wake si kwa matobo yale! namvua punde ingelinyesha..

wkt akilifikiria hilo mwanae alimgutua tena kwa kilio kilichoutonesha moyo wa mama yake,ambae mara hii aliupeleka mkono wake kichwani kwa mtoto wake nakutishwa kwa joto lililokuwa likipanda kwa kasi ktk mwili wa mwanae..
kitanda kilikuwa kichungu.. alipapasa huku na kule kuangaza kiberiti,sekunde
 
Utunzi huu ni hadithi au ushairi?
 
Back
Top Bottom