Uchaguzi 2020 Tuombe amani ya nchi yetu juu ya huu uchaguzi

Uchaguzi 2020 Tuombe amani ya nchi yetu juu ya huu uchaguzi

fathergetho

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
1,556
Reaction score
914
Salama wana JF?

Awali ya yote tujipe pole na pongezi ya kuyashugulikia maisha kwasababu bila ya hivyo basi tambua mkono hauta enda kinywani.

maada kuu pasipo ya kupoteza mda nadhani wote tunatambua what's goes around katika taifa letu nikiwa na maana ya uchaguzi mkuu wa kiti cha URAIS,WABUNGE NA MADIWANI (Bara na visiwani).

Huu ni wakati mwafaka wa Watanzania katika kumchagua kiongozi aliye bora, atakaye linda amani,atakaye leta maendeleo,atakaye tuongoza kwa haki na ukweli ulio na uwazi. Tutumie kula zetu vema kwa kumuomba mungu ili tusije tukajuta tukasema kama tungelijua tusingefanya haya.

Tunaitaji kiongozi atakayelinda amani kwa nguvu zake zote ili Watanzania tusije tukalia maana hakuna pakukimbilia, tumezoea kukaa kwa amani, tumezoea kusafili kila sehemu,amani imekuwa kitu cha msingi sana katika nchi yetu. Tumuombe Mungu atujaalie kuitumia kula yetu vema.

Eweee Rais utakaye kuja nakuombea kwa mwenyezi mungu kila la heri maana mamilioni ya Watanzania tunalia kwa ajili yako kwa maana wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho na kauli ya mwisho, namuomba mungu amuweke mlinzi kinywani mwako ili utoe maamuzi yaliyo sahihi ili Tanzania yetu isipoteze amani tuliyonayo utuongoze kwa amani katika kuleta mafanikio na kila mwananchi akapate kuyafurahia. Mwisho naitakia amani Tanzania naitakia amani afrika nawatakieni amani katika uchaguzi unaokuja.

MUNGU MWENYEZI ATUBARIKI

NB: AMANI YETU NDIO MAENDELEO YETU
 
Back
Top Bottom