Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.. Ukimaliza siku salama na kurudi kibandani kwako unamshukuru Mungu sana!
Ukikaa mahali lazima kwanza uangalie kushoto kulia mbele nyuma na ilibidi juu chini kama kuna sura zisizo za kawaida ziko nawe sambamba!
Ukipigiwa simu na namba ngeni ni shida pia.. Unakosa amani na kujiuliza kama hiyo simu ni ya kheri
Ukiendesha gari hali ni hiyohiyo.. Ni lazima kila wakati uangalie side mirrors na driving mirror kama hufuatiliwi..
Kupotea watu kumeongezeka
Kutekwa watu ndio kabisa.. Kusikia ya kwamba yule aliyepotea kaokotwa kafa si jambo la kustua sana tena!
Mwanzoni ilichukuliwa ya kwamba wakosoaji wa mfumo ndio wahanga wakuu lakini kwasasa tusidanganyane, yeyoye, popote na muda wowote linaweza kumkuta la kumkuta!
Sasa hivi hata mambo binafsi yameingizwa kwenye huo mfumo! Kuna wengine ni wahanga wa bahati mbaya na wengine ni wahanga kwa kusingiziwa tuu
Tulichodhani mwanzoni ni kuundiwa hofu, sasa ni kitisho dhahiri.. Ni kuwindwa kama mnyama!
Tuombeane sana sana tuweze kuumaliza mwaka huu salama maana hakuna aliye salama na kesho ni mbali kuliko jioni ya leo