Tuomboleze vifo vya wenzetu kwa matendo na si maneno

Tuomboleze vifo vya wenzetu kwa matendo na si maneno

Reinen herzens

New Member
Joined
Sep 25, 2025
Posts
1
Reaction score
1
Tusiomboleze wenzetu kwa maneno, tufanye vitendo
Wamekufa kwa sababu yetu, walitaka sisi wote tuishi kwenye nchi nzuri yenye uchaguzi huru na wa haki, uhuru wa vyombo vya habari, utawala wa sheria na sio amri za watu binafsi wanaojipa nchi kua mali zao, uwajibikaji wa viongozi na kuheshimu haki za binadamu.

Tufanye kila kitu ambacho kitaonyesha huzuni zetu. Tusiende uwanjani kushabikia timu za Tanzania, jezi zao na kadi za uanachama tuchome moto sababu wamechagua udhalimu badala ya haki.

Tusiende kwenye misiba au sherehe za wote wanaohusika kutuangamiza kuanzia wanajeshi, mapolisi, wasanii, waandishi wa habari yaani wote!

Unfollow account zote za wasanii, media, viongozi wa dini na watu wote mashuhuri wanaofumbia macho kuteketea kwetu Unsubscribe accounts zao za youtube.

Waliokufa na tulio hai wote lengo letu lilikua moja, tusiwasahau mapema mpaka haki waliyoifia ipatikane.

Damu zetu hazina thamani kushinda waliokufa wote tupo sawa.

Uoga hata hausaidii chochote! simnaona hata ambao hawakwenda kuandamano wengine pia wameuliwa kikatili?

Tujilinde lakini tusinunue uoga wanaotuuzia sababu tutazidi kuteketea na vizazi vyetu vitateketea.

Tusikubali kua wakimbizi nchini kwetu, pamoja tutajenga Tanzania imara✊
 
Back
Top Bottom