Kwa nchi kama ya kwetu ambapo sheria na katiba havifuatwi katika uendeshaji wa shughuli za kiutawala, uchaguzi hauheshimiwi, Tume za uchaguzi hazipo huru, Mahakama na Bunge vimefanywa kuwa idara za Serikali, na Rais amefanywa kuwa mfalme, ni muhimu sana kuwa na ukomo wa uongozi. Tena ni vema, uchaguzi ungekuwa unafanyika kila baada ya miaka 4, na ukomo wa lazima kipindi cha uongozi wa Rais mmpja iwe miaka 8. Miaka 10, ikitokea mmepata Rais wa hovyo, anakuwa ameharibu kila kitu.
Kama tungekuwa na katiba nzuri mpya, kama ile katiba pendekezwa ya Warioba, kukawa na Bunge huru, na tukawa na mahakama huru, kusingekuwa na haja ya kipindi cha ukomo wa Rais. Kwa sababu ikitokea Rais ni mbaya, ataondolewa kupitia uchaguzi. Akiwa hovyo sana anaweza kuondolewa hata kabla ya kipindi cha uchaguzi kupitia Bunge au mahakama.
Kwa sasa, kwa katiba yetu hii ya hovyo, na aina ya watawala tulio nao, na kwa chama hiki CCM kilichojaa mafisadi na watu wanafiki, NI MUHIMU SANA KUWA NA UKOMO WA LAZIMA KWA RAIS, TENA IKIWEZEKANA, UNGEPUNGUZWA NA KUWA MIAKA 8 BADALA YA 10.