Tuondoe term limit (mihula) kwenye uongozi, haina umuhimu wowote ule

Mtoa mada amekomalia tujitofautishe, Sasa tukishajitofautisha Kisha Nini? Yani hata Kama hakuna tija kwenye kujitofautisha? Kuna mjumbe amesema hata Marekani wenye mifumo imara bado wameona umuhimu wakuwa na mihula sembuse sisi wakanyaga Katiba. Hili kiufupi siyo wazo lenye afya hasa nyakati hizi labda kwa baadae.
 
Mwafrika na ustaarabu ni paka na panya!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Ni mawazo yake mleta mada, lakini ni wazo lisilo na mantiki, halina maana, na litaongeza matatizo ya kiutawala juu ya yale ambayo tayari tunayo.

Wazo la muhimu kwa sasa ni namna ya kuondokana na katiba hii ya hovyo tuliyo nayo, na sheria nyingine za hovyo, ikiwemo sheria ya uchaguzi ambayo inayofanya chaguzi zetu kutokuwa na maana.
 
Sio kwa nchi za Africa, hii mihula iliyopo tu watu bado wanajigeuza miungu watu mkiondoa mihula si ndio watajifany miungu wakuu kabisa.
 
Hayo ndiyo mawazo yenye tija kwasasa, Katiba mpya.
 
Unataka kumuongezea miaka ya kuongoza rais msikivu?
Kwa nini usimkamate yule anayesikilizwa na rais,umfanye kuwa rais?
 
Hatutaki mateso makubwa, yaani kwa katiba hiyo ya nyerere, uondoe term limit. Tutaamrishwa kulala saa 12 jioni. Yaani litakuwa kosa moja kubwa sana na hatutaki litokee. Yaani ungesema tupunguze term limit iwe miaka minne badala ya mitano hili kuwatia pressure viongozi wafanye kazi kwa umakini na hofu ya kuondoka mapema
 
Hata mifumo ya sasa bado sio kizuizi kwa watawala wengine kuamua kung'ang'ania madaraka Afrika.

Ni vyema tukaamua kujitofautisha na wengine japo ni ngumu.

Tuondoe term limit tuweke mifumo imara
Mifumo imara itangulie na baadae tuoñdoe term limits.
 
We nothing special, hebu twambie kwanza ni nani amekukonga katika uongozi wake hadi utushawishi kuondoa term limits. Kwangu Mimi hajatokea akitokea wananchi watapima, lakini siyo leo au kesho, tena kwa taasisi hizi dhaifu ambapo Rais anamkono kila sehemu; watabaki kuimba mapambio na kuwa kunguni baada ya kufuzu level ya uchawa.
 
Ondoa term limit halafu ukutane na wezi wa uchaguzi ala 2020 ndio tutajua maana ya term limit. Mola tusaidie na mawazo kama haya.
 
Wazo la kipuuzi kabisa kufungia mwaka[emoji29]
 
Naunga mkono hoja !!
Hii mihula ni kupoteza pesa za kuwatunza wakubwa wengi bila sababu yeyote ya msingi !
 
Sasa hapo ndipo suala la kuimarisha mifumo na taasisi nyengine unapo hitajika.
Mifumo na taasisi huongozwa na watu.
Tatizo ni baadhi ya watu ni wabaya na waovu, hivyo ni muhimu kuchuja waovu kama tunavyohakikisha kichaa hapati rungu, panga au silaha hatarishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…