Ukweli mtupu umenena ila,kwa weredi wake huo na ukubwa wa jina lake ulimfanya awe na kiburi,mfano wa kiburi cha Haji ni kufokea waandishi wa habari baadhi yao kuwaambia anatamani wasije kwenye press zake.
Kingine ni kutoa maneno machafu kwa bosi wake,lakini akuhishia hapo voice note yake ya pili anasema hivi"hawa watu ni wabaya sana wanaweza kuniwekea hata unga au kinifanyia kitu kibaya"hao watu wanaoweza kumfanyia Haji kitu kibaya ni Mo, Barbara na Hanspop au ni kinanani hao?
Ukweli usemwe licha ya mapungufu ya manara ila hawa waandishi wa habari kiukweli wana hila na chuki mbaya sana dhidi ya simba. Hapa manara alikua sahihi kuwaita takataka
Mtu kama kitenge na dauda hata humu wamejadiliwa sana kwa chuki zao wanazozionesha dhidi ya simba, kupitia tukio hili unaweza kuona ni namna gani swala hili la manara kwao limekua ni sherehe kubwa sana.
Imagine manara kaachia ngazi kwa maamuzi yake alafu headline ya kitenge kwenye tukio hilo la manara imesema MANARA ABWAGWA
Kero ya manara, ni mtu wa sifa sana na asiyeheshimu mipaka yake ya kazi. Kipindi kile mo dewj hafahamiki yuko wapi manara akajitokeza kama msemaji wa familia ya dewj.
Manara alithubutu kuingiza habari za siasa kwenye michezo huku akijua wazi timu iliyomuajiri inahusisha mashabiki kutoka pande tofauti tofauti za vyama.
Kuna siku manara alikua anaisifia simba akiifananisha mipango ya bechi la ufundi la simba kua ipo madhubuti kama chama cha mapinduzi. Hapa manara kaingiza siasa kwenye mpira kinyume na majukumu yake ambayo amepewa ayatimize kwa ajili ya club na mashabiki ambao wanatofautiana kivyama
Kingine huyu manara ni mkurupukaji, naamini kabla ya ku leak ile clip hakushirikisha ubongo ilikua ni mwemko tu ambao naimani baada ya hapo alijuta.
Alitegemea kuona support nyingi kwa upande wake kwa imani aliyojiaminisha kua anakubalika sana na wanasimba kwa kufananisha na mpinzani wake barbra ambaye ni mgeni
Kitu kingine nilichokiona kwa manara baada ya ku leak ile clip, nadhani alitegemea kuona MO atamsuport au kusema chochote ambacho kitam favor.
Na ndio maana alipoona kimya ni kama manara alichukia akawa anapost bidhaa za bakhresa kwa mfululizo kila wakati kama kumkomoa vile MO. Kuna post moja akitangaza maji ya uhai ya bakhresa aliandika caption kua "haya ndio maji bora na salama kuliko yeyote hapa tanzania"
Nadhani alifanya hivi ili kudhihaki maji ya masafi ya mo, nasema hivyo kwasababu hana kawaida ya kuandika caption yenye elements za kushusha bidhaa zingine especially kama hizo bidhaa pia MO anazo