Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Huyu hajibu hoja, unapoteza nguvu zako tu, ana unyani ule ambao mtikila alikuwa akiusema
 
Mkuu,
Mi nimesomea Uhandisi,
Nashangaa unavyoogopa kujibu maswali yangu wakati wewe una Masters ya uchumi na uwekezaji...

Anza kujibu, mi ntajibu yako yote...yani bila kupepesa..
 
Na
dhan ni mtaji
Leo oficini nimekaa mabos zangu wanapiga story kua kuna jamaa yao kaweka government bond kila mwezi ana milion 10 yake.
Alianzaga na milion 100
 
HAKUNA.
Kuwaambia hawa vijana waweke vibuku 10 vyao ili wawe matajiri ni Uongo mkubwa.

#YNWA
Ni wapi wameambiwa wawekeze wawe matajiri? Umemtolea mfano boda boda,ila nikukumbushe hata huyo boda boda anaweza kuwa na malengo kupitia hyo mifuko kwa kuchagua option ya kukuza mtaji wake. Hizo hizo buku 5 unazo ziponda akiziweka kwa nidhamu kwa muda wa miaka miwili anaweza kufikia malengo yake..
 
Kuna principle moja ya uchumi ya "the time value of money "
Yaani,Laki moja yako uliyonayo sasa ina nguvu kuliko laki moja utakayokuwa nayo mwakani....

Vitu hupanda bei kila mara,
Heri uweke laki UTT utakauta ongezeko la 10,000 ambayo itafidia upandaji wa bei ,,kuliko ukaificha ndani ya kabati ukaja kuikuta ipo vilevile.
 
Hizi hesabu ni za kilimo cha matikiti, uliza Kwanza spare parts na service ndio ujuwe gharama za uendeshaji wa vyombo vya Moto.
 
 

Attachments

Lakini baada ya hiyo miaka 30 fedha itakuwa imeporomoka thamani sana.
 
Hiki wengi wanakisahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…