MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ubarikiwe sana Mr Liverpool. Vijana waache uoga.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa na mimi nataka ninue tipper nifanyeje na nina uhakika wa kupata aftatu kwa siku ?Endelea kuweka hizo buku 5 huko kwenye mutual funds sijui shares sijui nini labda ipo siku tutakuona kwenye best investor in the country portifolio.!!
#YNWA
Huyu hajibu hoja, unapoteza nguvu zako tu, ana unyani ule ambao mtikila alikuwa akiusemaMkuu itoshe tu kusema HUNA UFAHAMU KUHUSU JAMBO ULILO LIANDIKA
Asilimia kubwa ya bandiko lako sio sahihi
Watu bado tuna mentality za kijamaa nadhani
Hii mifumo ni ya KIBEPARI na sio kwamba ni mifumo DHAIFU kwa TZ tu, we unataka uweka milioni yako uanze kulipwa mahela kibao?
Hizo asilimia za faida unazoziona ndio range ya faida dunia nzima tena wakati mwingine hapa bongo rate ni kubwa kuliko nchi zilizoendelea ili kuwashawishi watu wajifunze uwekezaji
Hata wewe ukitoka hapa uende USA na Milioni 10 zako ambazo ni sawa na Usd 3000+ huwezi kupata faida yoyote ya maana maana rate ni hizo hizo
Hivi mkuu unadhani kama unamiliki asilimia moja Vodacom au Barick utakua unamiliki kidogo?
Ukubwa wa faida unatokana na thamani ya kampuni mkuu
Hata ukiwa marekani halafu una hisa asilimia 80 ya kampuni uchwara utapata faida uchwara pia
Si sahihi kudhani thamani ya FB ni sawa na thamani ya JF
Hii sio mifumo dhaifu ya Kitanzania hii ni mifumo ya dunia nzima
Kwani financial market ya nje inaweza mfanya mtu awe tajiri ?Haya mwenye diploma turudi kwenye mada Je "Financial market ya bongo inaweza mfanya mtu mwenye kipato kidogo kuwa tajiri? "
Ni me state financial market, hivyo unaweza nipa mfano wa financial instrument yoyoteeee.
#YNWA
I agree lakini amepata experience awe makini next time.Mzee experience gani unaipata hapo??
Hizo ni hesabu, ukiweka hiki utapata hiki, ni calculated kabisa sasa hapo unatafuta uzoefu au unapoteza muda, elimu uliyopata ikusaidie kutopoteza muda kwa vitu usicyo na malengo navyo
Utajiri wao tunaona sisi masikini wa hapa Afrika ambayo tukiona mtu anaendasha VX tunamuona 1st class.Una uhakika na ulichoandika?
Mkuu,Ningefikiri unipe financial instrument moja, halafu uiteteee then unipe hata plan zake kwa bodaboda kuwa tajiri
Mi nishasema HAIPO, Nilidhani utanipa mfano ya kuwa "IPO" Ila naona umeishia personal attacks za elimu yangu..!!!
Ukiwa tayari kujibu mada bila ku-attack mtu KARIBU.
#YNWA
dhan ni mtajiINTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..
Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.
BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.
Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""
Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""
SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.
Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.
PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.
Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).
Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.
Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.
Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).
CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.
Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.
Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!
ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.
Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!
Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.
Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.
2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.
Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.
Tuendelee kutafuta pesa.
#YNWA
Ni wapi wameambiwa wawekeze wawe matajiri? Umemtolea mfano boda boda,ila nikukumbushe hata huyo boda boda anaweza kuwa na malengo kupitia hyo mifuko kwa kuchagua option ya kukuza mtaji wake. Hizo hizo buku 5 unazo ziponda akiziweka kwa nidhamu kwa muda wa miaka miwili anaweza kufikia malengo yake..HAKUNA.
Kuwaambia hawa vijana waweke vibuku 10 vyao ili wawe matajiri ni Uongo mkubwa.
#YNWA
Kuna principle moja ya uchumi ya "the time value of money "Kivipi?
Tatizo unakimbia maswali,,dhihirisha usomi wako mbele ya kadamnasi mkuu...
Hizi hesabu ni za kilimo cha matikiti, uliza Kwanza spare parts na service ndio ujuwe gharama za uendeshaji wa vyombo vya Moto.Wa Hindi wengi ni ma agent wa biashara wana tumika kuficha pesa za watakatishaji pesa wa kimataifa/mafisadi akiwa na pesa zake ana komaa na biashara tu, biashara zinalipa ila zina hitaji umakini, self devotion and presence na strategic planning ukiingia kichwa kichwa unaua mtaji.......
Kwa mfano 100m ukinunua tipper canter 3, kwa 35m each moja unaendesha mwenyewe mbili unawapa vijana kwa wiki kila moja huleta 350k mara 3 ni 1.05m × 4= 4.2m kwa Mwezi kwa mwaka 50.02m manaake 100 inakuletee faida ya 50m kwa mwakà hamna biashara ya finance market yoyote hapa TZ ya kukupa faida hiyo.
Government bond ni biashara ya Wahindi, anaweza kuweka B 1 BOT kila mwezi akavuta mshahara wa million kadhaa na pesa inazaa.
Kapuku na biashara ya pesa hakuna kitu kama hicho.
Mambo ya Forex na bit coin sijui ndio cryptocurrency achana nayo kabisa.
Nimemsikia Bongo zozo mara nyingi akidanganya watu kwamba Siri ya yeye kuwa na pesa ya kusafiri duniani ni bit coin, si kweli msiingizwe mkenge huo, wazungu ni fallen Angels huwezi kuujuwa undani wao.
Kwenye ujasiriamali ukiwa na roho ngumu na ukakomaa pesa unaweza kuiona, na kingine Bongo visource vya income unatakiwa uwe navyo vingivingi tu bila kusahau kujenga lodge, hii ndio biashara ya uhakika, starehe ya mafukara NI ngono.
Lakini baada ya hiyo miaka 30 fedha itakuwa imeporomoka thamani sana.hio weka mpunga sahau ata 30 years, ukishakua above 30 investment ya UTT bi kwaajili ya kusaafu kibos yan uneemeke at your 50s nakuendelea kwa saiv wewe invest kwaajili ya watoto wako wawe madon at their early 30s, kiufupi wewe hapo huusiki kabisa na benefit za hio mifuko kwa saivi kwenye kukokotoa interest rate time is the main factor ila wengi wana ignore hio
Hiki wengi wanakisahau.Kwa mfano wangu huohuo
Kuna utofauti Kati ya Compound interest ya Mkurugenzi/boss wako na mdada wenu wa kazi.
Jikite kwenye mada, hebu tengeneza schedule ya house girl kuwa tajiri kwa hizo compound interest akiwa na miaka 25.
Usisahau LIFE SPAN yetu.
#YNWA
Ndiyo maana kuna interest inayotolewa kila mwaka (8% mpaka 11%) ambayo inaenda kuzuia athari za mfumuko wa bei,,ambapo Tanzania ,3% mpaka 4%Lakini baada ya hiyo miaka 30 fedha itakuwa imeporomoka thamani sana.