Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Sijui Kama atakuelewa mkuu

Labda muulize hizo million mia angeweka utt Leo angekuwa na faida ya sh ngapi

Pia hiyo 2000 Dola moja ilikuwa 500tsh million 100
Sawa na Dola ngapi

Je Leo hiyo million 100 sawa na Dola ngapi ?
 
nahis BOT wanaelewa zaid yetu na ule mfuko upo chini yao tuache ujanjaujanja kwenye mambo ya kitaalamu ni kukaa na wataalamu na sio kutumia common sense kwenye mambo ya taaluma wao wanasemaga fact vs common sense
Bot wamejaa wstoto wa vigogo hamna think tank wa uchumi mle. Wangekua wsnajua Uchumi wasinge mruhusu JPm kufunga maduka ya kubadilishia pesa ambazo zilikua zina chochea flow of foreign exchange......
 
Uko sahihi purchasing power ya pesa inaenda ikipungua kwa sababu ya inflation.

Ila kwa mfano kama mtu anapokea 100k kwa mwaka haina maana yoyote ina maana ni kama analipwa 8k per month

Kwa cost of living za sasa haifidii chochote
 
Mkuu, kwa kifupi sio bongo tu. Dunia nzima financial market kwa mtu masikini haimfai. Hata Ulaya na Marekani, hakuna faida utakayopata. Lengo la financial markets sio kumtajirisha mtu (hizi UTTs na Faida) lengo lake ni kukutunzia pesa zako. Yaani hata ukizihitaji miaka 30 mbele utazipata kama zilivyo na kafaida kidogo. Mutual funds ni securities tu.

Ukitaka zi grow kafanye biashara mkuu.
Kwa kijana anaye hustle biashara inamlipa haraka, lakini kumbuka ikitokea mfano janga labda kaibiwa duka zima au duka limeungua moto anafilisika on the spot wakati yule wa mil 5 UTT hela yake ipo tu.

Kuwekeza hela UTT ni sehemu za kukuzia mitaji for future use sio kutajirika na huwezi kutajirika.
 
Utaua na kuridhika vyatosha Sana kukupa usingizi !!

Lakini kupata mapesa kibao Ili ule anasa kunachosha sana hasta usingizi hamna!!

Nahisi kati ya watu wanaoishi Kwa shida duniani ni matajiri!! Sidhani kama wanalala hao watu!!
Nahitaji sanaa pesa nyingi, huo usingizi wa shida poa tu acha uje.

#YNWA
 
Thanks.

#YNWA
 
Nikushauri "Diversify your portfolio through business"
Hakikisha una biashara ambayo hata kama haupo basi yenyewe inajiendesha.

Kuwa risk lover, hayo ya kukimbia risk achia wastaafu.

Fungua hardware, kuwa na depo, USA vifaa via electronics N.k Ila eti Mambo ya kumpa mtu mil 100 aje akupe mil 10 mwisho wa mwaka ni upuuuzi mtupu.

#YNWA
 
Mleta mada yuko sahihi, huwezi kuona multiplier effect ya bonds kwa uwekezaji wa hela za kuchungulia, bond price variation ina vary kwa less than 20+ or 15+ average kwa mwaka mzima.

The safest inv huwa naona bora ununue viwanja vinavyouzwa na halmashauri, vyenye vimepimwa na unakuwa na hati ya wizara kisha vipe hivo viwanja 5years to 10 yrs.
Ikipita lamitu huko umeula,, mfano kibada year 2007 sq 1300 ilikua worth 3m ila by 2020 you get yourself a clear 55m na simu za mdalali kila siku
 
Hapo mwisho umeuaaa…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…