Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Ndio maana masikini ataendelea kuwa masikini na tajiri ataendelea kuwa tajiri. Nani alikuambia ukiweka hela UTT unakua tajiri next day???? Hizo money market, shares and the like ni long term investment...pia elewa kwamba kila mtu ana malengo yake. Chagua kufanya kile kinachotimiza malengo yako.

Adios
 
Huyo jamaa ni mtu asiye jielewa mkuu. Wengi wanaweka akiba zao UTT kwa lengo la kukuza mtaji ili wafanye biashara baada ya miaka labda mitano. Hivyo badala ya kuweka pesa benk anaona aiweke UTT ili isipoteze thamani na baada ya miaka mitano aitoe. Ni wachache na wenye hela ndefu wanaweka hela UTT kwa lengo la kupata gawio la kila mwezi
 
Nimesema wapi unaweza tajirika na financial markets ? Hata unasema soko letu ni bado, je unafikiri bonds za huko nje ndio zinafanya watu wawe matajiri ?
 
Jamaa hapo kwenye biashara ya canter hesabu zake ametuingiza chaka.
Yaani ameassume hizo canter kwa muda wa mwaka mzima hazitapata breakdown yoyote yaani hata tairi hazitapasuka pancha[emoji3]
Mkuu gari kutoka japan used kama hiyo ni service tu na tayari na hizo ziko juu ya dereva, kama ni mwenye mali kununua inapasws dereva alete 420000 kwa wiki, viwanda vya tofari ndo vinakosisha hizo gari pesa ipo sio ya kusubiri, usiweke pesa yako UTT eti unasubiri faida za kijinga wekeza kwenye biashara baada ya mwaka utatoa ushuhuda hapa.
 
Nimesema wapi unaweza tajirika na financial markets ? Hata unasema soko letu ni bado, je unafikiri bonds za huko nje ndio zinafanya watu wawe matajiri ?
Kwamba nilicho comment hapo juu HUJAELWA?
Itakuwa we mjita, mkinga au muha braza.

Hakuna mtu hii dunia anaweza bishana na hizi kabilaa.

#YNWA
 
Biashara ndio KILA KITUU.

#YNWA
 
UTT AMIS sio uwekezaji wa mda mfupi upate utajiri wa haraka. Huu ni uwekezaji unaohitaji muda mrefu. Mfano walioanza kuwekeza 2005 Umoja fund thamani ya kipande ulikuwa 70 let's say mtu aliweka 70m at that time now thamani ya kipande ni 1007 it means angekuwa na 1bil now. Just imagine 19 years 1b sio ndogo. Muda ndo kila kitu kwenye uwekezaji.
 
Watakwambia pesa itakuwa imeshuka thamani, umepata hasara
 
Ni mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
 
Una ujinga wa kiwango cha juu sana.
Wewe unafanya nini Faida Fund?
""Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.
Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!""

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…