Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
Ndio maana masikini ataendelea kuwa masikini na tajiri ataendelea kuwa tajiri. Nani alikuambia ukiweka hela UTT unakua tajiri next day???? Hizo money market, shares and the like ni long term investment...pia elewa kwamba kila mtu ana malengo yake. Chagua kufanya kile kinachotimiza malengo yako.

Adios
 
Ndio maana masikini ataendelea kuwa masikini na tajiri ataendelea kuwa tajiri. Nani alikuambia ukiweka hela UTT unakua tajiri next day???? Hizo money market, shares and the like ni long term investment...pia elewa kwamba kila mtu ana malengo yake. Chagua kufanya kile kinachotimiza malengo yako.

Adios
Huyo jamaa ni mtu asiye jielewa mkuu. Wengi wanaweka akiba zao UTT kwa lengo la kukuza mtaji ili wafanye biashara baada ya miaka labda mitano. Hivyo badala ya kuweka pesa benk anaona aiweke UTT ili isipoteze thamani na baada ya miaka mitano aitoe. Ni wachache na wenye hela ndefu wanaweka hela UTT kwa lengo la kupata gawio la kila mwezi
 
Ngoja nikupe mfano:-

Kama unavyosema watu wasome documents za hizo bonds, kampuni na chochote wanachotaka kuwekeza kwenye money market ndio wawekeze wakiwa full informed basi hata kwenye biashara nako wafanye hivyohivyo.

Ila NGOJA nikupe mfano;

1. 2012 ndio niliajiriwa, nilivyoajiriwa nilikua bahili balaa na nilikuwa natunza sanaa pesa zako.

Kufika 2013 June nilienda mkoa Fulani nikanunua beach plot mil 3 (Eka 1)

Mwaka juzi (2022) nilipata simu kutoka kwa dalali ya kwamba kuna mzungu anaitaka anataka kunipa mil 40 ili nimuachie (anajenga hotel ya kitalii).
Jirani yangu (eka 5) aliuza Ila Mimi nimegoma, Ila nimegoma kwasababu ya bei.
Nilichofanya nimetafutia hati kuongeza thamani halafu nimevunga.

Kuna hela naitaka Ila mzungu bado kawa mbishi.

Hivyo namsubiri tu mzungu, najua hotel yake inazidi kuwa kubwa na eneo lake lina kuwa dogo hivyo ATAINGIA KINGI TUUUU....

NAOMBA NIAMBIE FINANCIAL MARKET GANI INGENIPA HIZI HELA KWA MIAKA HII 9?

2. Mshikaji wangu bwana 2015 alipiga mshindo akapata mil 15, fasta akaenda kununua nyumba Mwananyamala Dar.

Sasa bwana sasa hivi Mwananyamala ipo kwenye ule mradi wa CBD (Kama sijakosea jina) hivyo nyumba yake imezungukwa na rami pande mbili (lami za mtaani) na ipo kwenye kona.

Kuna mwarabu alimtafuta mwaka huu anataka kumpa mil 45 mwamba kakaza kasema ataiuza mwaka 2030 akiwa anastaafu (lengo lake ni kuacha kazi akiwa na miaka 40 (2030)) ili akaanze Mambo yake mapema. Malengo yake ni kufanya uwekezaji mkubwa kwenye biashara.

Sasa unadhani mwaka 2030 hii nyumba itakuwa na thamani gani ikiwa Leo watu wanaitaka kwa mil 45?

Mutual fund, share, and so forth WANAWEZA KUTOA KIASI KAMA HICHI kwa kipindi hicho?

Ushauri:-
Vijana wakiume wenye nguvu na akili, karibuni kwenye biashara acheni mambo ya kukimbia risk.

Njoo mjitose muone utamu wa biashara.

Hapa nilipo nataka kuuza hicho kuwanja/beach plot ili nifanye biashara ya kuwa wakala mkubwa sanaa wa gas za kupikia huu mkoa.

Let's think about risk vijana, mbona tuna wazee wetu waswahili wametufungulia njia, wakina R.I.P Mengi, Ruge, na Vunja Bei wangekuwa na akili hizi za kukimbia risk LEO WANGEKUWA WAPI, UNGEWAJUA WEWE KWA HAYA MAFANIKIO WALIYOYAPATA?

HEBU KIMBIENI NJOO KWENYE BIASHARA tukusanye pesa.

Akili hiyohiyo ya kusoma soma kwenye mabond huko na mashare ili upate high RR basi hiyohiyo akili na mbinu njoo uiapply kwenye biashara vijana.

#YNWA
Nimesema wapi unaweza tajirika na financial markets ? Hata unasema soko letu ni bado, je unafikiri bonds za huko nje ndio zinafanya watu wawe matajiri ?
 
Jamaa hapo kwenye biashara ya canter hesabu zake ametuingiza chaka.
Yaani ameassume hizo canter kwa muda wa mwaka mzima hazitapata breakdown yoyote yaani hata tairi hazitapasuka pancha[emoji3]
Mkuu gari kutoka japan used kama hiyo ni service tu na tayari na hizo ziko juu ya dereva, kama ni mwenye mali kununua inapasws dereva alete 420000 kwa wiki, viwanda vya tofari ndo vinakosisha hizo gari pesa ipo sio ya kusubiri, usiweke pesa yako UTT eti unasubiri faida za kijinga wekeza kwenye biashara baada ya mwaka utatoa ushuhuda hapa.
 
Nimesema wapi unaweza tajirika na financial markets ? Hata unasema soko letu ni bado, je unafikiri bonds za huko nje ndio zinafanya watu wawe matajiri ?
Kwamba nilicho comment hapo juu HUJAELWA?
Itakuwa we mjita, mkinga au muha braza.

Hakuna mtu hii dunia anaweza bishana na hizi kabilaa.

#YNWA
 
Mkuu gari kutoka japan used kama hiyo ni service tu na tayari na hizo ziko juu ya dereva, kama ni mwenye mali kununua inapasws dereva alete 420000 kwa wiki, viwanda vya tofari ndo vinakosisha hizo gari pesa ipo sio ya kusubiri, usiweke pesa yako UTT eti unasubiri faida za kijinga wekeza kwenye biashara baada ya mwaka utatoa ushuhuda hapa.
Biashara ndio KILA KITUU.

#YNWA
 
UTT AMIS sio uwekezaji wa mda mfupi upate utajiri wa haraka. Huu ni uwekezaji unaohitaji muda mrefu. Mfano walioanza kuwekeza 2005 Umoja fund thamani ya kipande ulikuwa 70 let's say mtu aliweka 70m at that time now thamani ya kipande ni 1007 it means angekuwa na 1bil now. Just imagine 19 years 1b sio ndogo. Muda ndo kila kitu kwenye uwekezaji.
 
UTT AMIS sio uwekezaji wa mda mfupi upate utajiri wa haraka. Huu ni uwekezaji unaohitaji muda mrefu. Mfano walioanza kuwekeza 2005 Umoja fund thamani ya kipande ulikuwa 70 let's say mtu aliweka 70m at that time now thamani ya kipande ni 1007 it means angekuwa na 1bil now. Just imagine 19 years 1b sio ndogo. Muda ndo kila kitu kwenye uwekezaji.
Watakwambia pesa itakuwa imeshuka thamani, umepata hasara
 
Ni mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
 
Una ujinga wa kiwango cha juu sana.
Wewe unafanya nini Faida Fund?
""Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.
Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!""

#YNWA
 
Back
Top Bottom