Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Hapo kwenye Bitcoin Bado Kuna namna uwekezaje wake unalipa. Mfano 2018 Bitcoin ilikuwa $3000. Kama ungenunua hata Bitcoin 3 tu Leo hii Bitcoin Moja ni $57,000 yaan return ya $54,000 kwa maika sita zidisha kwa coins 3 sasa.
 
Ni mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
Lengo lako Ni lipi? Kama Ni kukuza mtaji chukua mfuko wa liquid , Kama unataka upate visent kila mwezi (gawio) chukua Bond

Mimi Nadhani liquid itakufaa zaidi kwani mtaji wako Utakua kwa haraka kuliko kupata gawio
 
Shamba la hekari 100 ni sawa ila wizi wa aridhi ni mwingi sanaa litavamiwa tu,........ baada ya miaka 30 huenda ukabakiza hekari 1 au mbili kama hulitumii kulilima utakua umepoteza pesa bure bora uingie active bussiness
Mkuu shamba/viwanja kwa location nzuri inalipa return kubwa sana baada ya period of ten years.
Sharti utengezeze title deed pasivamiwe,
Then location iwe potential (jirani na mji mkubwa).
ukilenga location nzuri kwa ukapata heka kwanzia heka 50 wewe ni Tajiri wa miaka 20 ijayo
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Sidhani issue ya kuweka pesa utt ni kutafuta utajiri! Inaweza kuwa namna moja ya saving huku ukiokota hizo laki moja! Kuliko pesa ikae kwenye saving account ya benki. Mfano ukiweka 10M utt kwa mwaka unapata 1m.
10M inakupa 1M kwa mwaka (12months)
1,000,000/12=83,333 kwa mwezi
83,333/30=2,777 kwa siku

Unatumia milioni 10 kutengeneza Tsh 2,777 kwa siku

uko sahihi kwenye sentensi yako ya kwanza 'Sidhani issue ya kuweka pesa utt ni kutafuta utajiri'

Baada ya kufatilia mjadala kwa kina nmegundua kuwa kila mmoja yuko sahihi😂😂
 
changamoto kubwa tulionayo TZ hatufanyi reseach za kutosha kuelewa kitu kwa undan ili kujuwa kuwa kama kina align na malengo yetu..

inaonekana hujajua tofauti ya uwekezaji wa kwenye hisa.. nafikiri bado hujaelewa MMF na mifuko aina ya UTT zinafanyaje kazi.. huwezi kuwekeza UTT ukategemea milioni kumi yako ikupe faida ya milioni 5 kwa mwaka ndio maana inaitwa compounding interest.. UTT sio trading. investment .. inaelekea wewe lengo lako lililuwa trading investment.. so kulaumu UTT na FAIDA fund.. ni sawa na kununua tractor na kuilaumu haina speed ya V8. Land cruiser

Unasema TZ wanatoa faida ndogo.. hivi unajua MMF funds na index fund za ulaya na wanatoa percent ngapi za faida kwa mwaka.. UTT wanatoa average ya 10% - 12% ya faida kwa mwaka na kwa bongo kuanzia makampuni hadi kwenye masomo ya hisa average ya faida kwa mwaka ni kati ya 5% hadi 12%.. na hiyo ndio average ya return kwa sehem kubw duniani..

je niambie kama kuna nchi ambayo average ya return inazidi hapo tena Govt Bond za nchi tajiri unakuta inakupa max 5% wakat nchi za afrika Govt abond inakupa 10%+ ..
Anyway tukirudi kwenye hoja yako.. inaonekana uliwekeA UTT kwa lengo ambalo sio lengo la mfuko..

kwenye uwekezaji wa hisa kuna aina mbili je una target za uwekezaji wa mda mrefu au una target ya uwekezaji wa kutafuta faida kwa mda mfupi ambayo tunaita trading ( yaani numua hisa zikiwa bei ya chini kisha hisa zikipanda bei uza poga faida ngoja zikishuka numua tena subiri)

Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni mifuko ya uwekezaji wa mda mrefu ndio maana inaongelewa kuwa ni mifuko ya kuwekeza kwenye future yako kwa kujenga stability yako ya kifedha na familia yako taratibu.. ili uone faida kubwa ni lazima pesa yako iwepo walau 10yrs plus.. kama una mpango wa kukusanya mtaji tu ndio unaweza ukaitumia hii mifuko kama saving account huku ukiwa na uhakika inalinda thaman ya pesa yako tofauti na kuiweka bank.. ula kama unataka uifanye sehem ta uwekezaji wako kujenga utajiri then anzia kuhesabu 10yrs plus..

Tajiri mkubwa dunian warten Buffet utajiri wake ulikuwa kufikia bilion dollars kupitia hii mifuko ya dizaini hii.. na ukumbuke huyo amewekeza pia kwenye hisa za makampuni pia na hata kwenye startup nyingi..

Albert einstein alisema " , "Compound interest is the eighth wonder of the world. He who understands it, earns it. He who doesn't, pays it,"
 
Niliwa kueleza hili la hati fungani na fixed deposit kuwa kuna wakati na mazingira ni option nzuri kuliko kuanzisha biashara ambayo mtu hana uzoefu nayo kabisa na umri umekwenda

Waziri Mwigulu kaagiza zipatikane M200 ziwekwe kwenye hati fungani na mke wa marehemu awe anapokea kila mwezi interest kwaajili ya matumizi ya watoto kwa maisha yao yote hadi watakapo amua vinginevyo
 

Attachments

  • BF80BE90-6C34-461D-B87F-966B149E5BE1.jpeg
    271.8 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…