Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 6,958
- 16,358
- Thread starter
- #361
Wamekuwa wabishi kuelewa.Kiukweli kibongo bongo money market bado
#YNWA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamekuwa wabishi kuelewa.Kiukweli kibongo bongo money market bado
Fanya wewe mkuuSasa hiyo saving iingize kwenye hizo biashara nyengine ili hizo biashara ziwe kubwa zaidiii.
#YNWA
Hapo kwenye Bitcoin Bado Kuna namna uwekezaje wake unalipa. Mfano 2018 Bitcoin ilikuwa $3000. Kama ungenunua hata Bitcoin 3 tu Leo hii Bitcoin Moja ni $57,000 yaan return ya $54,000 kwa maika sita zidisha kwa coins 3 sasa.Government bond ni biashara ya Wahindi, anaweza kuweka B 1 BOT kila mwezi akavuta mshahara wa million kadhaa na pesa inazaa.
Kapuku na biashara ya pesa hakuna kitu kama hicho.
Mambo ya Forex na bit coin sijui ndio cryptocurrency achana nayo kabisa.
Nimemsikia Bongo zozo mara nyingi akidanganya watu kwamba Siri ya yeye kuwa na pesa ya kusafiri duniani ni bit coin, si kweli msiingizwe mkenge huo, wazungu ni fallen Angels huwezi kuujuwa undani wao.
Kwenye ujasiriamali ukiwa na roho ngumu na ukakomaa pesa unaweza kuiona, na kingine Bongo visource vya income unatakiwa uwe navyo vingivingi tu bila kusahau kujenga lodge, hii ndio biashara ya uhakika, starehe ya mafukara NI ngono.
Za kuambiwa changanya na zako""Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo""
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Band au liquidKuwekeza kwaajili ya baadae ndio maana nauliza ni mfuko upi mzuri kwa kuanza na 10M, UTT
Lengo lako Ni lipi? Kama Ni kukuza mtaji chukua mfuko wa liquid , Kama unataka upate visent kila mwezi (gawio) chukua BondNi mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
Kanunue hisa za CRDB, NMB, NICOL utakuja kunishukuru baadaeBand au liquid
Mkuu shamba/viwanja kwa location nzuri inalipa return kubwa sana baada ya period of ten years.Shamba la hekari 100 ni sawa ila wizi wa aridhi ni mwingi sanaa litavamiwa tu,........ baada ya miaka 30 huenda ukabakiza hekari 1 au mbili kama hulitumii kulilima utakua umepoteza pesa bure bora uingie active bussiness
Sahihi kabisa mkuuMleta mada yuko sahihi, huwezi kuona multiplier effect ya bonds kwa uwekezaji wa hela za kuchungulia, bond price variation ina vary kwa less than 20+ or 15+ average kwa mwaka mzima.
The safest inv huwa naona bora ununue viwanja vinavyouzwa na halmashauri, vyenye vimepimwa na unakuwa na hati ya wizara kisha vipe hivo viwanja 5years to 10 yrs.
Ikipita lamitu huko umeula,, mfano kibada year 2007 sq 1300 ilikua worth 3m ila by 2020 you get yourself a clear 55m na simu za mdalali kila sikuView attachment 2962859
10M inakupa 1M kwa mwaka (12months)Sidhani issue ya kuweka pesa utt ni kutafuta utajiri! Inaweza kuwa namna moja ya saving huku ukiokota hizo laki moja! Kuliko pesa ikae kwenye saving account ya benki. Mfano ukiweka 10M utt kwa mwaka unapata 1m.
changamoto kubwa tulionayo TZ hatufanyi reseach za kutosha kuelewa kitu kwa undan ili kujuwa kuwa kama kina align na malengo yetu..INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..
Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.
BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.
Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""
Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""
SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.
Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.
PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.
Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).
Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.
Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.
Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).
CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.
Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.
Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!
ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.
Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!
Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.
Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.
2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.
Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.
Tuendelee kutafuta pesa.
#YNWA
Niliwa kueleza hili la hati fungani na fixed deposit kuwa kuna wakati na mazingira ni option nzuri kuliko kuanzisha biashara ambayo mtu hana uzoefu nayo kabisa na umri umekwendaWatu wengi sana hatuna elimu ya haya mambo na ndio maana zinazalishwa zana nyingi sana za ajabu ajabu kama hizi
Shemeji yangu alifariki akaacha kama milioni 600 bank
Alikua na mke na watoto mapacha wawili.
Ukoo ulivutana sana nini kifanyike kuhusu na hizo hela
Mimi nikawashauri hela iwekwe Fixed acc bank iwe inatoa hela ya kujikumu hadi baadae tukitulia tutajua cha kufanya
makaka wakapinga sana kuwa huwezi kulaza hela nyingi hivyo bank ni UZEMBE
Mwisho wa siku ikaamuliwa
Mama mzazi apewe 50M.
Makaka 2 wapewe 100M wazungushe hela hadi watoto watakapo kuwa watu wazima
Mke wa marehemu akapewa 100M aanzishe biashara ya kujikimu
Halafu 300M ndio iwekwe fixed acc, rate yake ilikua 9.5%
Hapo kwa mwaka faida ni 28,500,000 na ikawa inagawanywa kwa miezi 12 ili ichukuliwe kila mwezi 2.3M
Baada ya mwaka tu mke wa marehemu biashara zake zote chalii 100M ikapotea.
Makaka wa marehemu ndio kabisa sijui walikwenda kununua mazao ikakatika 100M yote.
Sasa hivi familia ya marehemu wanaishi kwa kupokea 2.3M kila mwezi ya ile 300M kwenye fixed Acc, ndio pona pona yao vinginevyo wangeanza kuuza mali za marehemu
Watoto ndio kwanza wana miaka 10
Limepita AZIMIO hiyo hela asiguse mtu yeyote ibaki huko huko fixed Acc hadi watoto watakapo kwa watu wazima