Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Kwani mfano UTT ni mifuko miwili tu ndiyo inatoa gawio hiyo mengine minne, haitowi gawio.

Hivyo siyo kila anayeweka pesa uko ni kwa lengo la kupata gawio, binafsi nimeweka umoja ili nikuze mtaji wangu sasa utasemaje UTT ni mbaya ??
Hizo zote ni product za UTT
Aidha zitoe gawio ulichukue au uliache Ila ni gawio.

Endeleeni kunidanganya na returns za kina Mirambo Holdings tuu.
Umri unaenda.

Anzeni kupenda risk mkiwa bado vijana.

#YNWA
 
Umeanza tena maswala ya kujidanganya, kaingia rostam hapa.
Nimehudhuria semina nyingi sanaa za kina UTT na UMOJA FUND
Tatizo lao Hua wanapiga Mifano ya mamilioni
Utasikia "kwa miaka 7 ukiweka mil 100 utapata Mil 170"

Sasa hiyo mil 100 anamzungumzia bodaboda au Miramb holdings?

#YNWA
 
Kuna ukweli soko la mitaji Tanzania ni dogo sana kumbukeni tupo third world country najua Watanzania wengi hawataki kukubali hili lakini hii Nchi ni maskini kwenye dunia Bakhressa na Mo ni maskini. Hata hivyo kwa maisha ya kitanzania naona T/bonds zina afadhali kidogo pia msiogope kwenda kuweka pesa kwenye masoko mengine kama ya Kenya, Botswana na SA. Mkiweza nendeni hata Asia, Ulaya na US. Pia ndugu yangu Mtaji wa mil 40 siyo biashara kubwa usitosheke mapema.
 
Nimehudhuria semina nyingi sanaa za kina UTT na UMOJA FUND
Tatizo lao Hua wanapiga Mifano ya mamilioni
Utasikia "kwa miaka 7 ukiweka mil 100 utapata Mil 170"

Sasa hiyo mil 100 anamzungumzia bodaboda au Miramb holdings?

#YNWA
Umehudhuria mikutano mingi ya UTT na Umoja fund.
Umeudhuria mikutano ya wapi? Ipi?
Na kwanini waelezale vitu hivyo. Ndugu mimi ni kijana mdogo sana, ila hapa unanidanganya. Matapeli ndio uongea hivo, yaani mkutanoni upewe kauli ya hivo. Acha bwana. UTT asset management na investor service hawafanyi vikao vya kihuni hivo.
Na kila mwaka wanatoa taarifa ya liquid fund yako mwaka jana wametoa november. Haiwi kihuni hivo boss. Embu tulia si kila kitu cha kuropoka hadharani
 
Hutakiwi kujibizana na watu wapumbavu mkuu. Save your Energy please..huyo hayupo tayari kuelewa
 
Tafuta watu wakujibu mkuu kuna watu hawana finance literacy just ignore, watakutoa kwenye mada yako, ni wacheche wa kuelewa tu, mke wangu alinunua hisa NmB za 2m miaka 15 nyuma lakini mpaka leo hajawahi kupokea hata 500,000 kwa mwaka mimi nilio wekeza kwenye biashara ndo nimemuajiri tena... Finance market haowezi kutoa mtu kwenye umasikini ila inaweza kuendeleza wenye nacho sio masikini
 
Ukishakuwa na cash 500 millions huwezi kubali kuweeka pesa yako kwenye faida ndogo kama hiyo ya Utt
Kiufupi labda uwe na pesa zilizopatikana kwa wizi na deals huko serikalini au uwe mstaafu uliyelipwa billions.
 
unauhakika kozi ulisomea uchumi mkuu? compounding interest unaielewa vyema inavyo piga kaz there is no wonder ulipigwa forex inaonekana unapenda utajir wa chap kitu ambacho kimewaponza kina meek mill
Boda boda anawekesa kiasi gani Utt ili naye aishi kibos akistaafu.?
Mada ni simple tu, unaicomplicate! Soko la pesa Sio kwa kila mtu in fact ni kama lipo kwa ajili ya matajiri tu. Haiingii akilini niweke 10 mil Utt halafu nisubiri faida ya 1 mil baada ya mwaka! Ila tajiri anaweza subiri gawio la 100mil kwa mwaka kama kaweka 1 billion utt.
 
Nimehudhuria semina nyingi sanaa za kina UTT na UMOJA FUND
Tatizo lao Hua wanapiga Mifano ya mamilioni
Utasikia "kwa miaka 7 ukiweka mil 100 utapata Mil 170"

Sasa hiyo mil 100 anamzungumzia bodaboda au Miramb holdings?

#YNWA
Wako sahihi kupigia hio mifano maana hao ndio targets wao! Wewe bukuonaire na lakionaire mkae pembeni😂
 
Ukishakuwa na cash 500 millions huwezi kubali kuweeka pesa yako kwenye faida ndogo kama hiyo ya Utt
Kiufupi labda uwe na pesa zilizopatikana kwa wizi na deals huko serikalini au uwe mstaafu uliyelipwa billions.
500m ni mtaji wa kuanzisha micro finance au credit facility nzuri tu katika semi urban area na kua na tellers wswili, kama loans za short period1moth to 6 months uki-charge kwa 22% intrest rate, ndani ya mwaka moja unaweza ukawa na annual turnover 1.5bn manaake kwa mwaka unaweza ukatengeneza faida ya 700m both in assets and cash.

Sasa kws watu wanao jua finance banking kwanini uweka pesa yoko kwenye marketing Finance, labda kama ya wizi au betting.
 
Wizara ya fedha ikiwa na semina Dodoma kwa watumishi, huwa wanaalikwa hao UTT na FAIDA FUND Kuja kutoa elimu.

Ila tuishie hapo.

Okey ma - investor, investment is the marathon not a race.
🤣🤣🤣🤣
Angalieni isije ikawa ni race mnakimbizana na wakenya..!!

Anyway:-
Karibuni kwenye biashara
Risk Lovers, YESS WE ARE.

#YNWA
 
Utaipataje ukiwa kijana wakati babaako hana influence yeyote chamani😂
 
Hio 22% unayopigia hesabu ni kwa hawa hawa wabongo naowajua mimi au utaifanyia maeneo ya Norway?😂
 
Pia ndugu yangu Mtaji wa mil 40 siyo biashara kubwa usitosheke mapema.
Sijaridhika ndio maana ya kununua FUSO.
Nanunua Fuso kwasababu kuna "Market share" Nimeiona sehemu hivyo naona ili kuipata linatakiwa FUSO.

Kwahiyo hii plan tu ya kununua FUSO ni kwamba Ninataka kukuza biashara.

#YNWA
 
Mada ni nzuri ila nimesoma kama comments 20 za mwanzo naona wengi wanashindwa kutofautisha biashara na uwekezaji. Kwenye biashara always tunategemea faida ya haraka lakini uwekezaji faida ni ndogo inayoweza chukua muda mrefu. Hizi UTT na Gov Bonds wanauchumi wakubwa wanaziita ni securities.

Kwahiyo unapoweka hela UTT means unafanya kwa ajili ya ulinzi wa pesa yako lakini ukitegemea kwa matumizi ya baadae. Mfano wewe mleta mada unasema unatunza pesa UTT ili uje ununue tipper tofauti na kwamba hii pesa ungekua umeiweka bank tu. Lakini neno security linakuja ku apply zaidi pale utakapo chukulia mkopo manunuzi ya tipper badala ya kununua cash. Hivyo UTT inabaki kukulinda hata pale majanga yatakapo tokea.

Ni kweli kwa nchi kama yetu hizi faida yake ni ndogo lakini bado zinasimama kama the best securities kwa waTZ wengi kulinda pesa zao. Kwa nchi nyingine wanafaidika sana kutokana na nchi hizo kuwa stable kiuchumi.
 

Attachments

  • Screenshot_20220922-124152.png
    120.6 KB · Views: 37
Boss investing is not getting rich, getting rich is a result
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…