Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo


Ni kweli, huwezi toka kimaisha kwa mutual funds Hapa Bongo.UTT na Faida fund ni kwamba wanalinda fedha yako isipungue thamani. Faida wanayotoa ni ndogo. Kama umepata mahali 10m, chukua 5m piga biashara zingine weka UTT au faida fund.Halafu baada ya mwaka hiyo 5m yako ya kwenye biashara itakuwa imeliwa nusu kwa sababu ya kujifunza biashara.Ndiyo uende ukachukue hiΓ½o 5m iliyobaki maana hapo utakuwa umeshaijua biashara yako vizuri kabisa pamoja na changamoto zake

Hizo funds zinataka uwe na hela nyingi ili uweze kuona faida yenye maana.

sababu nadhani roughly ni 10% pa ndiyo faida yake.

so ili uweze kupata income ya sh 3m kwa mwezi inakubidi uweke sh.360milion.

Unaweza ukawa una hayo malengo ya muda mrefu,kwamba unaweka kidogo kidogo mpaka zifikie kiasi ambacho kitaanza kukipa reasoble monthly income.

Huwa ni sawa na mtu anayejenga nyumba kwa sababu ya kupangisha,faida yake ni ndogo pia bora anayejenga na kuuza.
 
15000 kwa mwaka sawa na 150K, hio ni sawa 1.5M kwa miaka 10 na ni sawa na around 5 Million kwa miaka mitatu.

Million 5 kwa UTT ambayo around 10% kwa mwaka sawa na gabion la 500,000 Tzs (Laki tano tu kwa mwaka) ambayo sawa na kamshahara kagawio ka around 50,000 kwa mwezi

Uwo utajiri wa kutisha upo wapi hapo


UTT ni sehemu kwaajiri ya wenye Dedham kuhifadhi pesa ambayo hawaitaji kuitumia kwa wakati huo na kupitia kuweka kwao wanapewa zawadi za gawio waendelee kunywa juisi
 
Uweke 15000 kila mwezi kwa miaka 30.mfululizo!!! , naomba kujua age na sayari unayoishi!! Naamini sio Dunia hii ninayoijua
 
Mimi nawekeza UTT kwa sababu ya kukusanya mtaji huku hela ikiwa inaongezwa kwa riba nzuri kuliko zile Fixed na Bonus account za mabenk.
Kwa mwenye mtaji mdogo huko UTT patumieni kama sehemu ya kuweka akiba sio kuwe kama Investment
Tusio na mamilioni, najua UTT tunasave pesa. Kumbe kuna wanao save kwa ajili ya kupokea faida iendeshe maisha 😁

Anyway… tunaendelea kuzirushia UTT chenji zote ambazo hatuzitumii kwa sasa… zitatufaa baadaeπŸ’₯
UTT AMIS Inategemea Na Aina Ya Bidhaa Uliyoichagua Lakini Kwa Kutunza Cash Bila Pressure Ni Kuzuri Na Kama Wadau Waliochangia Ukiiacha Kipande Kinapanda Ingawa Taratibu
Banks Shida Yao Pesa Inakatwa Mpaka Unabaki Mdomo Wazi Kama Umekamatwa Ugoni


Ni Kweli Masoko Ya Fedha Tanzania Yanaathiliwa Na Kuzorota Sana Kwa Shilingi
Ila Ingekuwa Pesa Yetu Inaimarika Mambo Yangekuwa Safi
 
Hii nadharia ni nzuri sana.very linear!
 
pigia compound interest ulete jibu narudi punde with facts and figures
 
nyie hesabu mnapigaje wazee?
 
Uweke 15000 kila mwezi kwa miaka 30.mfululizo!!! , naomba kujua age na sayari unayoishi!! Naamini sio Dunia hii ninayoijua
uko na limited knowledge sana hamtaki kujifunza kutoka kwa wazee wenu
 
Mlioweka hela utt mlivomshambulia jamaaa sasa[emoji3]

Ukiweza kutofautisha hivi vi4 utagundua kila mtu anakuwa amefanya best decision kwake
1. Business vs investment
2. Active vs passive
3. Mtu mwenye muda na nafasi ya kuwa active kwenye biashara vs asiye na muda kabisa, probably kaajiriwa
 
Sawa soko letu la Financial market ni dogo,lakini mkuu...

1.Unasema Bongo hakuna kampuni ambayo ukimiliki 1% ukatajirika ,una uhakika na ulisemalo ?

2.Una ubavu wa kumiliki hisa 1% ya makampuni haya CRDB,NICOL,TWIGA,SWISSPORT,NMB,TCC na TBL...

3.Je,huyo wa boda kuweka millioni mbili chumbani mwaka mzima na kuweka millioni 2 katika fixed deposit au UTT ,kipi ni bora...

4.Financial markets za Bonds,Mutual funds ni za low risk, so unategemea ziwe na faida kubwa kama biashara?

5.Binafsi nina mashaka na Elimu yako hiyo uliyosema,
Yani ulitaka utajairike kwa return ya 8 hadi 11% annually, huku umeweka 5million ,πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ina maana hata hesabu haujui ama ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…