Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA

Ni kweli, huwezi toka kimaisha kwa mutual funds Hapa Bongo.UTT na Faida fund ni kwamba wanalinda fedha yako isipungue thamani. Faida wanayotoa ni ndogo. Kama umepata mahali 10m, chukua 5m piga biashara zingine weka UTT au faida fund.Halafu baada ya mwaka hiyo 5m yako ya kwenye biashara itakuwa imeliwa nusu kwa sababu ya kujifunza biashara.Ndiyo uende ukachukue hiýo 5m iliyobaki maana hapo utakuwa umeshaijua biashara yako vizuri kabisa pamoja na changamoto zake

Hizo funds zinataka uwe na hela nyingi ili uweze kuona faida yenye maana.

sababu nadhani roughly ni 10% pa ndiyo faida yake.

so ili uweze kupata income ya sh 3m kwa mwezi inakubidi uweke sh.360milion.

Unaweza ukawa una hayo malengo ya muda mrefu,kwamba unaweka kidogo kidogo mpaka zifikie kiasi ambacho kitaanza kukipa reasoble monthly income.

Huwa ni sawa na mtu anayejenga nyumba kwa sababu ya kupangisha,faida yake ni ndogo pia bora anayejenga na kuuza.
 
ukiweka 15000 kila mwez kwa miaka 30 , mwingine akaweka 30,000,000 kila mwez kwa miaka mitano amin usiamin huyu alieweka kidogokidogo muda mrefu ataoneoka na ukwasi wakutisha kuliko huyu milionea
financial illiteracy ndio iliotamalaki humu huwez kutegemea hela ya utt ulipie kodi mwakani kaeni vizuri na wenye uelewa wa hii kitu msikurupuke
15000 kwa mwaka sawa na 150K, hio ni sawa 1.5M kwa miaka 10 na ni sawa na around 5 Million kwa miaka mitatu.

Million 5 kwa UTT ambayo around 10% kwa mwaka sawa na gabion la 500,000 Tzs (Laki tano tu kwa mwaka) ambayo sawa na kamshahara kagawio ka around 50,000 kwa mwezi

Uwo utajiri wa kutisha upo wapi hapo

UTT ni sehemu kwaajiri ya wenye Dedham kuhifadhi pesa ambayo hawaitaji kuitumia kwa wakati huo na kupitia kuweka kwao wanapewa zawadi za gawio waendelee kunywa juisi
 
Uweke 15000 kila mwezi kwa miaka 30.mfululizo!!! , naomba kujua age na sayari unayoishi!! Naamini sio Dunia hii ninayoijua
 
Mimi nawekeza UTT kwa sababu ya kukusanya mtaji huku hela ikiwa inaongezwa kwa riba nzuri kuliko zile Fixed na Bonus account za mabenk.
Kwa mwenye mtaji mdogo huko UTT patumieni kama sehemu ya kuweka akiba sio kuwe kama Investment
Tusio na mamilioni, najua UTT tunasave pesa. Kumbe kuna wanao save kwa ajili ya kupokea faida iendeshe maisha 😁

Anyway… tunaendelea kuzirushia UTT chenji zote ambazo hatuzitumii kwa sasa… zitatufaa baadae💥
hio weka mpunga sahau ata 30 years, ukishakua above 30 investment ya UTT bi kwaajili ya kusaafu kibos yan uneemeke at your 50s nakuendelea kwa saiv wewe invest kwaajili ya watoto wako wawe madon at their early 30s, kiufupi wewe hapo huusiki kabisa na benefit za hio mifuko kwa saivi kwenye kukokotoa interest rate time is the main factor ila wengi wana ignore hio
Hizo utt/faida, shares nk ni kwaajili ya uwekezaji wa muda mrefu, yaani after from 10 yrs na kuendelea ndio unaenjoy sio unaweka leo unataka faida kesho, yaani hizo ni za kula hapo mbeleniiii, kama unataka za muda mfupi then fanya biashara, nakumbuka miaka mitano iliyopita niliweka 10mil benk Moja hivi fixed, after six month faida laki mbili hahaha nikaitoa, kwahiyo ukiwekeza kwenye hizo money markets hutakiwi kuwa na haraka nazo weka then tulia,endelea ukiwekeza taratibu..halafu pia Kuna watu wengine hawawezi kabisa kufanya biashara so ndio maana anawekeza huko coz hataki stress ingawa kijifaida kinakua taratibu...kupanga ni kuchagua
UTT AMIS Inategemea Na Aina Ya Bidhaa Uliyoichagua Lakini Kwa Kutunza Cash Bila Pressure Ni Kuzuri Na Kama Wadau Waliochangia Ukiiacha Kipande Kinapanda Ingawa Taratibu
Banks Shida Yao Pesa Inakatwa Mpaka Unabaki Mdomo Wazi Kama Umekamatwa Ugoni

Ni Kweli Masoko Ya Fedha Tanzania Yanaathiliwa Na Kuzorota Sana Kwa Shilingi
Ila Ingekuwa Pesa Yetu Inaimarika Mambo Yangekuwa Safi
 
Wa Hindi wengi ni ma agent wa biashara wana tumika kuficha pesa za watakatishaji pesa wa kimataifa/mafisadi akiwa na pesa zake ana komaa na biashara tu, biashara zinalipa ila zina hitaji umakini, self devotion and presence na strategic planning ukiingia kichwa kichwa unaua mtaji.......

Kwa mfano 100m ukinunua tipper canter 3, kwa 35m each moja unaendesha mwenyewe mbili unawapa vijana kwa wiki kila moja huleta 350k mara 3 ni 1.05m × 4= 4.2m kwa Mwezi kwa mwaka 50.02m manaake 100 inakuletee faida ya 50m kwa mwakà hamna biashara ya finance market yoyote hapa TZ ya kukupa faida hiyo.
Hii nadharia ni nzuri sana.very linear!
 
15000 kwa mwaka sawa na 150K, hio ni sawa 1.5M kwa miaka 10 na ni sawa na around 5 Million kwa miaka mitatu.

Million 5 kwa UTT ambayo around 10% kwa mwaka sawa na gabion la 500,000 Tzs (Laki tano tu kwa mwaka) ambayo sawa na kamshahara kagawio ka around 50,000 kwa mwezi

Uwo utajiri wa kutisha upo wapi hapo

UTT ni sehemu kwaajiri ya wenye Dedham kuhifadhi pesa ambayo hawaitaji kuitumia kwa wakati huo na kupitia kuweka kwao wanapewa zawadi za gawio waendelee kunywa juisi
pigia compound interest ulete jibu narudi punde with facts and figures
 
nyie hesabu mnapigaje wazee?
UTT AMIS Inategemea Na Aina Ya Bidhaa Uliyoichagua Lakini Kwa Kutunza Cash Bila Pressure Ni Kuzuri Na Kama Wadau Waliochangia Ukiiacha Kipande Kinapanda Ingawa Taratibu
Banks Shida Yao Pesa Inakatwa Mpaka Unabaki Mdomo Wazi Kama Umekamatwa Ugoni

Ni Kweli Masoko Ya Fedha Tanzania Yanaathiliwa Na Kuzorota Sana Kwa Shilingi
Ila Ingekuwa Pesa Yetu Inaimarika Mambo Yangekuwa Safi
 
Uweke 15000 kila mwezi kwa miaka 30.mfululizo!!! , naomba kujua age na sayari unayoishi!! Naamini sio Dunia hii ninayoijua
uko na limited knowledge sana hamtaki kujifunza kutoka kwa wazee wenu
 
UTT amis calculator ipo google hebu ingieni humo muelimike ili muache kuita watu freemason mkiona wamekua matajiri uzeeni
Screenshot_20240412-211003.png
Screenshot_20240412-211329.png
Screenshot_20240412-211341.png
Screenshot_20240412-211357.png
 
Mlioweka hela utt mlivomshambulia jamaaa sasa[emoji3]

Ukiweza kutofautisha hivi vi4 utagundua kila mtu anakuwa amefanya best decision kwake
1. Business vs investment
2. Active vs passive
3. Mtu mwenye muda na nafasi ya kuwa active kwenye biashara vs asiye na muda kabisa, probably kaajiriwa
 
INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
Sawa soko letu la Financial market ni dogo,lakini mkuu...

1.Unasema Bongo hakuna kampuni ambayo ukimiliki 1% ukatajirika ,una uhakika na ulisemalo ?

2.Una ubavu wa kumiliki hisa 1% ya makampuni haya CRDB,NICOL,TWIGA,SWISSPORT,NMB,TCC na TBL...

3.Je,huyo wa boda kuweka millioni mbili chumbani mwaka mzima na kuweka millioni 2 katika fixed deposit au UTT ,kipi ni bora...

4.Financial markets za Bonds,Mutual funds ni za low risk, so unategemea ziwe na faida kubwa kama biashara?

5.Binafsi nina mashaka na Elimu yako hiyo uliyosema,
Yani ulitaka utajairike kwa return ya 8 hadi 11% annually, huku umeweka 5million ,😂😂😂 ina maana hata hesabu haujui ama ?
 
Back
Top Bottom