Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Nyie hizi biashara waachieni wenye mamilioni.
Mirambo Holdings (Rostam) anamiliki hisa asilimia 35 za vodacom.

Unadhani alianza na buku huyu..!!

#YNWA
 
Jibu maswali yangu kwanza....hapa ni hoja kwa hoja.
Ndiyo mjadala wa kiungwana unavyoenda.
Ningefikiri unipe financial instrument moja, halafu uiteteee then unipe hata plan zake kwa bodaboda kuwa tajiri
Mi nishasema HAIPO, Nilidhani utanipa mfano ya kuwa "IPO" Ila naona umeishia personal attacks za elimu yangu..!!!

Ukiwa tayari kujibu mada bila ku-attack mtu KARIBU.

#YNWA
 
Omeongea point sana mkuu,,,
Binafsi nafkiri mleta mada Alitakiwa ajue hilo....
Kifupi kama umeelewa mada yangu nimekwambia..
Active income/business income is the best than the passive income.

Hizi passive income "Making money while sleeping" sio njema kwa mafukara, mtu huwezi kumpa mil 2 yako halafu baada ya mwaka akakupa 200k kama faida halafu ukasema "You were making money while sleeping"

Ila sasa wale wahindi na wachaga akina Mtei wale sasa ndio are making money with there money(s) in the market..!!

#YNWA
 
Nipongeze mjadala mzuri Sana ,
Ni moja ya Uzi wa great thinker

Nimejaribu kufuatilia muwekaezaji mkubwa kwenye Soko la Dse
Ambaye ni Patric Schegg
Kwenye bank ya Nmb anamiliki asilimia moja point nane 1.8
Sawa na na mtaji wa sh bill 55.
Mtaji wa Nmb unakadiriwa zaidi trilioni moja na billion 200

Labda tunaweza kupata picha kuchambua zaidi

Gawio la Nmb 2023 lilikuwa billion 143
Kwa MTU mwenye asilimia moja gawanya kwa 100

 
Mkuu itoshe tu kusema HUNA UFAHAMU KUHUSU JAMBO ULILO LIANDIKA
Asilimia kubwa ya bandiko lako sio sahihi

Watu bado tuna mentality za kijamaa nadhani
Hii mifumo ni ya KIBEPARI na sio kwamba ni mifumo DHAIFU kwa TZ tu, we unataka uweka milioni yako uanze kulipwa mahela kibao?

Hizo asilimia za faida unazoziona ndio range ya faida dunia nzima tena wakati mwingine hapa bongo rate ni kubwa kuliko nchi zilizoendelea ili kuwashawishi watu wajifunze uwekezaji

Hata wewe ukitoka hapa uende USA na Milioni 10 zako ambazo ni sawa na Usd 3000+ huwezi kupata faida yoyote ya maana maana rate ni hizo hizo

Hivi mkuu unadhani kama unamiliki asilimia moja Vodacom au Barick utakua unamiliki kidogo?
Ukubwa wa faida unatokana na thamani ya kampuni mkuu
Hata ukiwa marekani halafu una hisa asilimia 80 ya kampuni uchwara utapata faida uchwara pia
Si sahihi kudhani thamani ya FB ni sawa na thamani ya JF

Hii sio mifumo dhaifu ya Kitanzania hii ni mifumo ya dunia nzima
 
Haya mwenye diploma turudi kwenye mada Je "Financial market ya bongo inaweza mfanya mtu mwenye kipato kidogo kuwa tajiri? "

Ni me state financial market, hivyo unaweza nipa mfano wa financial instrument yoyoteeee.

#YNWA
 
Wait Explain it
 
Hii inabidi uanze mara baada ya kuajiriwa na tena uwe na financial mentor (wa bure lkn[emoji3]) unayemsikiliza na kumheshimu hasa

Otherwise ile mihemuko ya kuanza kushika hela yako mwenyewe utataka ujaribu kila kitu, uwe kila mahali, ununue kila unachokifikiria kichwani hata kama hukihitaji; hutoboi[emoji23]
 
1.Unaposema soko la fedha si salama..
-je ,una maana kuna wizi au utapeli kwenye hilo soko
-Litamfanya mtu aingie hasara?
-Je ,soko la fedha Marekani na Ulaya ni salama kuliko Bongo...?

2.Umeponda soko la fedha,lakini hapohapo umeweka fedha kwenye FAIDA ili ununue FUSO,
-Je,unawapotosha wenzako ili ufaidike wewe tu.
-Kwanini unaendelea kuweka fedha kwenye mutual ?

3.Kuhusu hisa,
-Haujui kuwa bei za hisa zinashuka na kupanda ama?
-Je,bei ya hisa kushuka ili athiri gawio?

4.Katika hao wawili watakao powa hizo millioni 5,
-Ni yupi ana nafasi kubwa ya kupoteza hizo millioni 5 zote,kama hasara ikitokea...
 
Kwahiyo tunakubaliana kwamba kwa kijana anayejitafuta Leo "Financial market ya bongo sio sehemu yake sahihi ya kuanzia maisha ya kujitafuta?"

Kumwambia mtu aweke 2mil FAIDA FUND au Anunue hisa za Vodacom basi ni Bora akawe mchuuzi k.koo na hizo mil 2?

#YNWA
 
Endelea kuweka hizo buku 5 huko kwenye mutual funds sijui shares sijui nini labda ipo siku tutakuona kwenye best investor in the country portifolio.!!

#YNWA
Mkuu labda ungetoa ushauri pia

Mtu akiweza kupata hiyo buku 5 kila siku labda ni boda boda, unamshauri afanyeje?
 
Kwa mlio isema vibaya FOREX ma CRYPTOCURRENCY naombeni futeni kauli zenu. Kama hujui kuhusu hivyo vitu omba uelekezwe.

Ulipoteza 200$ kwa IQ OPTION sijui, sasa kule si ni kubet tuu, app ile imaweza hata saidia kufanya analysis.

Uliwahi soma mambo ya fundamental analysis kabla ya kufungua trades zako ?!

PLEASE PLEASE soma kuhusu forex ma CRYPTOCURRENCY ndiyo uende ukawekeze, tena KUWEKEZA SIYO KUCHEZA AU KUFANYA FANYA.

Tuwe na discipline.

FOREX NDIYO INA NILISHA, KUNIVISHA, KULIPA KODI LAKI 2 kWA MWEZI NA NMEWEKEZA KILIMO CHA MAHINDI JEKA 10 KITETO.

FOREX NDIYO IMENIPA JEURI HATA KAZI SINA MIDA WA KU APPLY TENA SABABU NILITESEKA MNO NA KUOMBA AJIRA,DHARAU NA MISHAHARA MIDOGO NDIYO ILIPELEKEA KUANGALIA NINI NIJIFUNZE NIPATE HELA KAMA EXTRA INCOME.

Nime hangaika sana na online jobs huko UPWORK mpaka nilipo kuja kutana na Forex.
Kwa namna moja ama nyingine forex ili nifelisha sana mpaka kujuta kuijua ila sikukata tamaa sababu kuna rafiki yangu niliwahi soma naye 1 mpaka form 4 nilikutana naye kwenye semina, hana kazi ua kuajiriwa anafanya forex na ana life zuri tuu.

Anyway story ni ndefu.

IT TOOK ME 4 YEARS OF STRUGGLE MPAKA LEO HII I SAY THANK YOU FOREX KWA KUNIHESHIMISHA.

About Cryptocurrency pia ni lazima ujifunze kujua coin ipi ni mpya au projects gani imeleta coin mpya sokoni, projects ipi iko ma wwtu wengi kiasi, ni valid yaani siyo fake etc ndiyo unune coin yake au kuwekeza.

SHIDA MTU AKIAMBIWA TOA HELA UFINDISHWE HAUTAKI NENDA SOKONI UKIPIGWA ZA USO UNARUDI UNASEMA FOREX NI FAKE GAME AND GAMBLING.

THat is your side of story but to me I LOVE FOREX KULIKO HATA DEMU WANGU.

CRYPTOCURRENCY TO THE MOON 🚀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…