Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Ni mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
Nini malengo yako ?
 
INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA

Umenena hasa
 
Ni mfuko gani unaofaa UTT AMISS kwa mwekezaji anayeanza na 10M, kati ya bond fund na liquid fund ili angalau kukuza uwekezaji na kwa uwekezaji huo faida yake ipoje?
Bond fund ...kuna gawio + ongezeko la mtaji
 
[/QUOTE
Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho
Hii ingekuwa practical analysis isiyo na tone la mashaka.
 
Sidhani issue ya kuweka pesa utt ni kutafuta utajiri! Inaweza kuwa namna moja ya saving huku ukiokota hizo laki moja! Kuliko pesa ikae kwenye saving account ya benki. Mfano ukiweka 10M utt kwa mwaka unapata 1m.
Kimbilia risk
Njoo tufanye biashara.

#YNWA
 
Tafuta watu wakujibu mkuu kuna watu hawana finance literacy just ignore, watakutoa kwenye mada yako, ni wacheche wa kuelewa tu, mke wangu alinunua hisa NmB za 2m miaka 15 nyuma lakini mpaka leo hajawahi kupokea hata 500,000 kwa mwaka mimi nilio wekeza kwenye biashara ndo nimemuajiri tena... Finance market haowezi kutoa mtu kwenye umasikini ila inaweza kuendeleza wenye nacho sio masikini
Amen.

#YNWA
 
UTT amis calculator ipo google hebu ingieni humo muelimike ili muache kuita watu freemason mkiona wamekua matajiri uzeen.

Kwahiyo kiongozi unasubiri uwe tajiri uzeeni?

#YNWA
 
Nilishasema humu kitambo, hizo biashara za UTT na bonds ukitaka uone pesa walau uwe na 500M ama zaidi ya hapo. Otherwise wenye hizo million 5 mpaka 10 fanyeni uchuuzi tu. You will make more money that way kuliko kusubiria gawio la laki hadi laki 5 mwisho wa mwaka.
Kumbe UTT ni biashara na hamsemi?
Wengine ni sehemu ya kutunzia saving zetu.
Na ni bora kuliko kuilaza NMB.
 
Inaonekana hata Hisa ajui ni nini pia na tofauti zake 1% ya NMB ufanyi kazi milele unakula bata tu kila kiwanja
Aha,hapo nimekuelewa,,
Ila binafsi nina mashaka na elimu ya mleta mada...
Yani kasoma uchumi,halafu anasema Bongo hakuna kampuni ambayo ukimiliki 1% ya hisa zake ni inaleta mshiko mrefu...
Dah ,arudishe vyeti vyote.

Mwenye 1% ya hisa za NMB unamjua ni nani?
Ukichunguza sanaa utakuta ni yuleyule aliyepata mabilioni nje ya money market akaja kuwekeza.

Hivyo hela yake hakuipata money market.

Ndio manaa nakwambia "Hivi soko la pesa ni la mafukara kweli?""

Rostam (Mirambo) ndio major shareholder wa Vodacom, hizo hela za kuwa major share holder alizipata wapi?

#YNWA
 
Kumbe UTT ni biashara na hamsemi?
Wengine ni sehemu ya kutunzia saving zetu.
Na ni bora kuliko kuilaza NMB.
Madam kwanini uzifiche huko

Njoo nazo huku mtaani tupige deal

#YNWA
 
Yani nakaa nafkiria kama alikuwa anaingia darasani kweli...
Kumiliii 1% ya hisa ni anachukulia simple...

Kwenye Bonds,sijui hata anafuagiliaga za huko nje, dah...!?
Ngoja aje uone, tutatukanwa mpaka basi.

Hizo hela za kumiliki hiyo 1% kazipata wapi?

Unadhani huyo anayemiliki 1% ya NMB na NBC alianzia na buku 10 yake?

Alizitafuta kwenye biashara akazileta money market.

Na huu ndio msingi wa mada hiii yoteee.

#YNWA
 
Nipongeze mjadala mzuri Sana ,
Ni moja ya Uzi wa great thinker

Nimejaribu kufuatilia muwekaezaji mkubwa kwenye Soko la Dse
Ambaye ni Patric Schegg
Kwenye bank ya Nmb anamiliki asilimia moja point nane 1.8
Sawa na na mtaji wa sh bill 55.
Mtaji wa Nmb unakadiriwa zaidi trilioni moja na billion 200

Labda tunaweza kupata picha kuchambua zaidi

Gawio la Nmb 2023 lilikuwa billion 143
Kwa MTU mwenye asilimia moja gawanya kwa 100

View attachment 2961875View attachment 2961876
Hizi hela za kuwekeza hivi alizitoa wapi?

#YNWA
 
INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
Umeeleweka...
 
Faida ya uwekezaji inategemea na riba yako. Pesa ikiwa nyingi kwa asilimia ndogo tuh ya riba faida yako itakuwa kubwa.

Kwa hiyo juwa asilimia ya riba kwa pesa yako unayowekeza ni shs ngapi afu kisha ndo utathmini je itakufaa au laa!
 
Back
Top Bottom