Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Tuongee ukweli: Soko la pesa la Tanzania (UTT, Hisa N.k) haliwezi kukufanya ukawa tajiri kwa mtaji wako mdogo

Mwenye 1% ya hisa za NMB unamjua ni nani?
Ukichunguza sanaa utakuta ni yuleyule aliyepata mabilioni nje ya money market akaja kuwekeza.

Hivyo hela yake hakuipata money market.

Ndio manaa nakwambia "Hivi soko la pesa ni la mafukara kweli?""

Rostam (Mirambo) ndio major shareholder wa Vodacom, hizo hela za kuwa major share holder alizipata wapi?

#YNWA
Umeelewa hoja ulizojibu??
 
Kwa mfano 100m ukinunua tipper canter 3, kwa 35m each moja unaendesha mwenyewe mbili unawapa vijana kwa wiki kila moja huleta 350k mara 3 ni 1.05m × 4= 4.2m kwa Mwezi kwa mwaka 50.02m manaake 100 inakuletee faida ya 50m kwa mwakà hamna biashara ya finance market yoyote hapa Tanzania ya kukupa faida hiyo.
hesabu za Alinacha hizo, hakuna biashara ambayo ina risk kubwa kuliko hiyo ya magari. Halafu unadhani dereva atakuletea hizo fedha kirahisi sana. Mimi nilishafanya biashara ya gari la fuso, trekta na hata uber na vyote niliishia chali!
 
hesabu za Alinacha hizo, hakuna biashara ambayo ina risk kubwa kuliko hiyo ya magari. Halafu unadhani dereva atakuletea hizo fedha kirahisi sana. Mimi nilishafanya biashara ya gari la fuso, trekta na hata uber na vyote niliishia chali!
Tatizo mnakimbia haraka changamoto.
Changamoto zikabili USIKIMBIE

#YNWA
 
INTRODUCTION.
Mr. Liverpool kwa maisha ni mfanyakazi, mfanyabiashara na mmiliki wa vipande kwenye mutual fund..

Nasoma(ga) sanaa watu humu wanasifia FOREX, Mutual Funds (hasa UTT), Government bonds and bills na fixed deposits.

BODY:-
Soko la pesa Tanzania sio kubwa kiasi kwa maana kuna hisa, vipande vya mutual fund, government bonds and bills, na fixed deposit.

Ila nachojiuliza ""Hivi kuna mtanzania mwenye kipato kidogo anaweza ishi vizuri kwa kumiliki chochote hapo juu?""

Kuna ukweli mwingi sanaa huwa hausemwi na wataalamu wa finance and investment, ""Je soko letu ni sahihi kwa watu masikini na kipato cha kawaida??""

SCENARIO:-
Mimi binafsi ni muwekezaji wa mutual fund inayoitwa FAIDA FUND inayosimamiwa na Watumishi Housing kupitia Wizara OR - Tamisemi.
Nina vipande 25,768.9364 nilivyoanza ununuzi tokea June/2023.

Lakini pia nina biashara kubwa tu mjini yenye mtaji wa Mil 40 na assets za mil 15.

PROBLEM.
Changamoto ya soko letu la pesa ni faida yake ambayo ni ndogo sanaaa...
1. Nilishawahi miliki hisa za Vodacom na CRDB, nilikaa nazo mwaka na nusu, ilinichukua miezi mitatu kuziuza. Hiki ndicho kilichonikera balaa na kuachana na mambo ya hisa.
2. Nikaingia UTT Amis, wale jamaa walikaa na pesa yangu mwaka wakanipa 100k kama Faida..!!
3. Nikaingia kwenye forex nako nikapigwa 200 dollar yoteee (kupitia IQ Option).
4. Nikawaza Crypto currency ila sikushiriki.

Wakati nateseka na money market nilikuwa tayari nina hii biashara iliyoanza kwa mtaji wa mil 10 (bidhaa Mil 5 na Assets 3 na maandalizi mil 2).

Wakati huo wotee biashara ilikuwa inakuwa na wateja wanamiminika Ila money market ilikuwa tu inasumbua na kuiweka hela yangu idle.

Nilivutiwa na money market kwasababu ya
1. Elimu yangu ya chuo, nimesoma Economics, Finance and Investment kwa Diploma, Bachelor na Masters yangu.
2. Ujana, kutaka kuwa tajiri
3. Kuona kazini napoteza muda.

Kwasasa nipo na FAIDA FUND tu japo naona performance yake inazingua tuuuu (slowly growing).

CONCLUSION:-
Kifupi soko la fedha la kibongo bado ni nogo sanaa na si salama kwa kijana mtafutaji.

Yaani, si rafiki kwa kijana ambae anajitafuta akapata mil 2 yake eti akawekeza ili atoke kimaisha, na ni tofauti sanaa na wenzetu.

Wenzetu ukisikia mtu anamiliki 1% ya hisa za facebook huyu ni tajiri balaaa, ila hebu nitafutie mtanzania anayemiliki kampuni 1% ya share akawa tajiri...!!!

ANYWAY:-
Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.

Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!

Hivyo FAIDA FUND naifanya kama bank account ya malengo yangu..!! ila sio NJIA YA KUNITOA KIMAISHA.

Na kiukweli:-
1. Money market ya bongo ni kwa ajili ya watu waoga na wasio na muda wa kufanya biashara Ila nyie wenye mioyo migumu NJOONI KWENYE BIASHARA TUPAMBANE.
Biashara ina hela balaaaaa.

2. Money market ya bongo ni kwaajili ya matajiri tu, yaani jitafutee kwenye biashara halafu "diversify your portifolio" kwa money market, Ila sio eti umepiga deal la mil 5 halafu unaingia money market ili Uwe tajiri, aiseee HAIPO.

Watakaokwambia biashara ni high risk hebu....
1. Waulize kuhusu hisa za NICO, JATU, TOL
2. Waulize kuhusu Vodacom, waliingia DSE kwa 1000/share ghafla wakashuka mpaka 800/share..!!
3. Waambie hivi, watokee watu wawili wasio na ajira wote wapewe mil 5 each, mmoja aende UTT na mwengine aende Kariakoo kuwa winga halafu baada ya mwaka tuje na mrejesho.

Tuendelee kutafuta pesa.

#YNWA
Hili linawafaa sana wastaafu wetu
 
Tatizo mnakimbia haraka changamoto.
Changamoto zikabili USIKIMBIE

#YNWA
hamna, fuso mwanzo dereva anakuletea fedha nzuri unaona mambo yanakwenda sawa. Akishakaa muda anaanza kufikiria kuwa anakugawia wewe hizo fedha bure bure tu husahau kwamba lile fuso siyo la kwake. Na hapo ndipo mtanange unapoanza, atakuletea laki nne atakwambia inahitaji matengenezo laki tatu, siku nyingine akwambie hakupata mzigo na kila aina ya visingizio, mwisho unapiga hesabu unaona faida ni minus.

Pia nilikuwa na trekta nimenunua jipya na jembe lake miaka mitatu nimeishia kupata kama milioni kumi na nikaona isiwe shida wacha niliuze angalau nipate hicho kidogo, kwani hata fedha zangu za mtaji hazikurudi.
 
Pia wazoefu watueleze system ya UTT inatoa percent siku za kazi tuu yani (Mon - Fri) au ni siku zote haijalishi ni w/end au public holidays ,Me nna hisi mambo mawili 👇🏻

Moja

Inawezekana system yao haifanyi kazi siku za w/end na public holidays lakini percent ya hizo siku inakuja kuingia siku ya week itakayofuata

Mbili

Inawezekana system yao imelenga kutoa percent kwa siku za kazi tuu yani (Mon-Fri)

Wenye uzoefu zaidi watakuja kutupa mwanga
 
15000 kwa mwaka sawa na 150K, hio ni sawa 1.5M kwa miaka 10 na ni sawa na around 5 Million kwa miaka mitatu.

Million 5 kwa UTT ambayo around 10% kwa mwaka sawa na gabion la 500,000 Tzs (Laki tano tu kwa mwaka) ambayo sawa na kamshahara kagawio ka around 50,000 kwa mwezi

Uwo utajiri wa kutisha upo wapi hapo


UTT ni sehemu kwaajiri ya wenye Dedham kuhifadhi pesa ambayo hawaitaji kuitumia kwa wakati huo na kupitia kuweka kwao wanapewa zawadi za gawio waendelee kunywa juisi
Elimu elimu elimu , mwingine huyu hapa , ila wabongo bhana - kitu kimoja kila mtu kwasababu kaenda shule basi anadhani anaweza akajibu kila kitu, tujikite kutafuta maarifa sahihi ndio tujibu hoja.
 
Kwa watumiaji wa Tigo Pata GB za bure kwa kufuta maelekezo haya.



1. Ingia TigoPesa app (Kama hauna download play store)

2. Ingia Invite & Earn

3. Bonyeza Redeem

4. Weka hii code 2ZJVO8ZK

Baada ya hapo utapata 2GB na DK kibao bure kabisa!!
 
""Mimi nipo FAIDA FUND kwasababu BONUS Account ya NMB imeshindwa kunipa nachotaka. Bonus Account ili upate interest inatakiwa upambane hasaaaaaa.
Kwasasa nina mpango wa kununua fuso niwe napeleka mizigo kijijini, hivyo nawekeza FAIDA FUND ili ikifika hela ya bei ya fuso basi nitoe ninunue hiyo gari iingie mzigoni...!!!""

#YNWA
Mkuu kwanini ulichagua Faida Fund na sio UTT? Faida Fund ni nzuri kuliko UTT?
 
Elimu elimu elimu , mwingine huyu hapa , ila wabongo bhana - kitu kimoja kila mtu kwasababu kaenda shule basi anadhani anaweza akajibu kila kitu, tujikite kutafuta maarifa sahihi ndio tujibu hoja.
Haelewi kuhusu compound interest ila "tunaongelea compound interest ya hisa za rostam Voda au za mlala hoi NMB??""

#YNWA
 
Back
Top Bottom