Mkuu
GlobalCitizen, sku nyingine ukirudi mwanza hakikisha unarudi msimu wa ngoma za NYABHULEBHUA huwa ni around mid June to July. Aisee nilienjoy sana huu msimu na ni bure kabsa hakuna kiingilio. Kiufupi ni ngoma za kisukuma wakipiga kushindana ngoma bora ya mwaka, sasa utam wa ngoma kwa mtazamaji hauishii kwa kuangalia jinsi wanavyocheza na Mdundo wa kiasli pekee bali Kuna burudani nyingine ya ziada pale unapoona WASHINDANI WAKILOGANA LIVE BILA CHENGA.
Aisee askuambie mtu. That is the best cultural tourism ever experienced, huko gamboshi watakusimulia tu habari za kusadikika na pia wale leaders wanaikanusha sana hii kitu so unaweza usipate undani wake kiivyo, sehem ambayo hutajutia ni kwenye hizo goma maana kulogana ni moja ya tamduni zao ili upate watazamaji wengi wa ngoma yako na hatimae utangazwe mshindi mshindi.
Nilishuhudia nyao za watu zikikaangwa kwenye sufuria, kuku akinyonyolewa manyoa huku wazee wakimunenea lugha isiyoeleweka, jamaa mchafuu anamakucha na manywele mengi akitembea uwanjani watu wakadai huyo ni mskule. For sure zile ngoma sjui ni kwa hazitangazwi. Zinachezwa Kisesa karibu kabsa na makumbusho ya Bujora kwenye uwanja wao wanauita uwanja wa ngome. Hata hizo ngoma za Bujora unazikutana kwenye mashindano na wanapadri wao wanaloga huyo hatari, ni mashindano ya ngoma zote kutoka sehem mbali mbali za waskuma, Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Geita. One week shows, aisee ni hatari
Some few pics of events
Sorry kila nikiaload picha naambiwa something went wrong, contact admin