Wakati Msanii Dudubaya ana "trend" na msemo wake waarufu wa kulinda migongo, baadhi ya watu walibeza, wengine waliona kama ni kauli za kilevi levi na wengine waliona kama mtu anayetafuta kiki
Baadae kauli ikapokelewa na baadhi ya watu wanaojua ukubwa wa tatizo alilokuwa ameligusa Dudubaya; yaani ushoga
Baadhi ya viongozi wa serikali wakamtaka akajieleze mbele yao, wengine wakamtaka apunguze ukali wa maneno, vyombo vikubwa vya habari vika mu-ignore
Hayo yote hayakuondoa ukweli wa alichokisema, kwamba ushoga una shamiri na hali ni mbaya jamii isipochukua hatua vijana wataharibika zaidi
Sasa mashoga wameamua kuja hadharani!
Wanafanya makongamano, wanahojiwa, wanafanya party, wanajieleza wamefikaje hapo na wengine wanasema wako tayari kwenda kutetea haki zao mahakamani
Kauli ya Dudubaya imewafanya wajisikie wanyonge, wajione wakosaji, dhalimu na watu wasio faa! Sasa wameamua kuja kujitetea
Swali ni moja tu; jamii itaweza kuwadhibiti?
Sasa mmeona ukubwa wa tatizo au bado mnapingana na Dudubaya?
Serikali je? Bado mnakigugumizi cha kukataa au kukubali kuwa tatizo lipo?