Tupambane kabla ya miaka 40

Tupambane kabla ya miaka 40

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

MAISHA SI YA BABAAKO

Maisha bana raha sana, haswa ukiwa unayaishi vile unataka au unatamani wewe. Japo yana changamoto zake, hatukatai ila unazikabili vipi. Maisha ni yako wewe mwenyewe, si ya Babaako. Pigana jitahidi utafute chakwako, pigana utafute na cha wanao, wakija wakute maisha yana unafuu, wakute maisha mazuri. Life Begin at 40? Achia wazungu huo msemo mana tumeshindwa utafsiri. Wao wanamaanisha ukiwa na 40 ndo uwe unakula maisha.

Wanamaanisha uwe unaishi maisha sio unajaribu kusindikiza maisha, unakua tayari una elimu unayoihitaji ya kutosha, unakua tayari una vyanzo vya hela vingi, uwe na familia yako, uwe kwako na sio umepanga, uwe na usafiri wako binafsi. Huku sijui hata tunautafsiri vipi huu msemo, Mana wengine at 40 ndo tunasoma badala ya kuwa tunasomesha watoto, at 40 ndo tunawaza biashara na kujaribu hiki na kile na vyote vinafeli, at 40 ndo tunawaza kuoa au tumeoa juzi kati tu na ndoa inayumba kama mlevi wa Chimpumu, at 40 hatujawahi hata kwenda pata exposure mbugani au nchi za jirani, tukitoka sana tunatoka sinza kwenda lodge k/nyama na kurudi afta wiki, wengine at 40 bado tunaomba nipige tafu nyumbani.

We endelea kujiita popo mla ujana, ati unakula bata mpaka saa nane unaingia insta unalike picha ya Diamond akiwa studio saa saba usiku, wakati mwenzako anatengeneza pesa. Voda net ikiyumba unalalamika kana kwamba unatumia internet kutengeneza pesa kumbe unasoma na ku-like tu Post za umbea. Kazi kutupostia picha za mafuriko, mara gari imegonga treni, mara picha za team makorokocho. Ila kumbuka at 40 utakua una-like maisha ya wenzio. Kwa sasa,
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
Instagram Account follow: Elimu_biashara
 
Last edited by a moderator:
Naona ulikua na hasira hadi umemunda ili utueleze
 
Back
Top Bottom