Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Naomba kwa mwenye usahihi wa tuhuma zinazoelekezwa kwa shahidi Na. 8 atusaidie kuziweka hapa for future reference lakini pia kusaidia familia yake kujua kijana wao huko kazina anatumikia umma au anajitumikia. Hadi Sasa zipo tuhuma tatu nzito dhidi yake ambazo Ni:
1. Anatuhumiwa kumwekea mtuhumiwa wa Kwanza kwenye kesi ya Mbowe Bastola katika lengo lakufanikisha kubambikiwa kesi. Taarifa hizi Ni kwa mujibu wa mtuhumiwa wakati anajieleza wakati wa pingamizi
2. Akiwa OC CID Arusha anatuhumiwa kupokea mgao wa fedha za unyang'anyi zilizoporwa na Sabaya. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa shahidi kwenye kesi iliyopelekea sabaya Kufungwa
3. Anatuhumiwa kushirikiana na aaskari wenzake kumwekea Prof mmoja pembe za ndovu kwenye mzinga na Kisha kumkamata profesa huyo na kumweka ndani akidai atamfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi jambo lililopelekea Profesa kuwapa yeye na Askari wenzie milioni Mia Moja kufukia kesi hiyo. Baadaye taarifa zilivuja na profesa kuhojiwa na vyombo vya habari na kukiri kukamatwa na Askari wa upelelezi USA RIver ambapo Bw. Jumanne ndiye alikuwa mkuu wa upelelezi. Ni vigumu kumtenganisha OC CID na upelelezi ofisoni kwake na kumbuka yeye ndiye aliyelekeza mzee huyo kuwekwa mahabusu na kuruhusu vijana wake kwenda na mtuhumiwa Hadi benki kuchukua fedha.
Wakati tunajadili tuhuma hizo, taarifa zinadai alisimamishwa kazi kwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili japo Hadi Sasa TAKUKURU awajachukua hatua yoyote dhidi yao. Aidha hakuna uchunguzi wowote uliofanywa kuhusu uhusika wake kwenye uhalifu wa Sabaya.
Hawa tuseme ndio wakubwa wa nchi hii, wanakupa kipigo wanapigiwa makofi kwa kazi nzuri.
Mwenye kupingana na taarifa hizi au Mwenye ilufafanuzi zaidi karibuni, Mimi haya Ni kwa mujibu wa yaliyopo mitandaoni na hapa ni mtandaoni twende kazi