Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mimi toka Dar hadi musoma aisee nilikuwa mwoga hatari spidi niliyokuwa naenda nayo ni 40/50 yaani nikifika 60 naona kama naenda mtaroni,break zilikuwa kila wakati halafu nikajichanganya kupita barabara yaarusha nilitumia siku 3.
Mimi toka Dar hadi musoma aisee nilikuwa mwoga hatari spidi niliyokuwa naenda nayo ni 40/50 yaani nikifika 60 naona kama naenda mtaroni,break zilikuwa kila wakati halafu nikajichanganya kupita barabara yaarusha nilitumia siku 3.
Sana tulipofika geti la ngorongo kuna dereva wa basi akanifuata kuniuliza mbona break nyingi sikumjibu kwasababu ukweli nilikuwa naujua mwenyewe maana nilikuwa learner.Utakua ulipigiwa horn za kutosha na kupigwa mataa mengi sana, kwa mwendo huo highway!!!
Wewe hutufai asee yan speed 60 kwenye highway ndio maximum? 😂😂 hiyo ni speed ya kuendeshea katikati ya mji mkuu.Mimi toka Dar hadi musoma aisee nilikuwa mwoga hatari spidi niliyokuwa naenda nayo ni 40/50 yaani nikifika 60 naona kama naenda mtaroni,break zilikuwa kila wakati halafu nikajichanganya kupita barabara yaarusha nilitumia siku 3.
Utakuwa umetumia petroli lita mia kwenda tuSana tulipofika geti la ngorongo kuna dereva wa basi akanifuata kuniuliza mbona break nyingi sikumjibu kwasababu ukweli nilikuwa naujua mwenyewe maana nilikuwa leaner.
Daaaah,umefika nyumbani kwetu mkuu,Masasi moja hiyooooo,big up sana,na wewe ni wa huko huko nn au mishe tu za nchini?Dar Masasi nilidamka saa kumi na moja nilitumia siku nzima mpaka mishale ya saa kumi jioni. Nilifika miguu imevimba na mabega yanauma utadhani nililibeba mgongoni. Gari ni gx 100.
Aisee ni story ndefu,nilikuwa nimeagiza gari nje ya nchi,nikawa katika kujipanga kwenda kuifuata jamaa yangu ambae kwao wana gari akaniambia anauwezo wa kuendesha,kwa hiyo tukapanga safari usiku wa safari jamaa ananiambia haioni leseni(alikuwa hana kumbe)na mimi nimeshakata tiketi ikabidi tuondoke,nikajakugundua kumbe pia sio mzoefu wa kuendesha kwa hiyo mimi nilikuwa na leseni ikabidi ndio niwe dereva tegemeo ingawa sina uzoefu na highway,kwa hiyo unaweza kuelewa kwanini nilitembea speed hiyo.
Angalia kwenye matairi ya gari yako yanakuaga na recommendations za maximum speed.Me kwa mara ya kwanza nilitoka Arusha to Dar nikiwa na familia, natumia Runx speed ya 80 -120. Sijui ujasiri ulitoka wapi aisee na road kulikuwa na mvua, nakumbuka nilitoka sa12 nikafika Dar sa9 mchana. Ninampango wa kwenda tena December hii pamoja na familia tena.
Kuna mdau hapo juu kasema yeye alitumia Runx speed kali hadi ikabast. Kwa anayejua recomended speed kwa gari kama hii ukiwa highway ni kiasi gani maana wengine ufundi wa magari hatuujui sana kama nikipata shida huko road.
Ndio kila jambo lina faida na hasara zake,faida ni kwamba baada ya pale nilipata ujasiri wa kuendesha highway nikawa sihitaji dereva ninapokwenda safari ndefu.[emoji23]so kilichotokea ni bora hata angebaki maana kazi uliifanya yote wewe? Ila speed 60 mwendo wa kinyonga sana
Utadhani umetembea kutoka Mwanza hadi DSM kumbe hapo Masasi tuDar Masasi nilidamka saa kumi na moja nilitumia siku nzima mpaka mishale ya saa kumi jioni. Nilifika miguu imevimba na mabega yanauma utadhani nililibeba mgongoni. Gari ni gx 100.
Mimi safari yangu ya kwanza ilikuwa ni kutoka Kigoma-Morogoro.Hapo ni baada ya kupata uzoefu wa Mwezi mmoja wa kuendesha gari baada ya kujifunza kupitia tutorials za youtube.Nilitoka Kigoma saa 12 asubuhi.Kutokana na uoga niliokuwa nao,nilipanga kwamba nitatembea maximum mwendo wa 70km/hr.
Nilikuwa na kigari changu,Carina Si nikiwa nimepakia abiria wanne,mkononi nina leseni yenye umri wa wiki 1 tu.Aisee,asikwambie mtu,nilijikuta huko njiani nime-gain confidence ya ajabu,mwendo ulikuwa ni 150,160....nikipunguza sana ni 100/120.Nilikuwa sitaki kuona basi au lorry mbele yangu,ni mwendo wa kuzikata tu.Nilijikuta saa 10 jioni niko dodoma city,nikapumzika kama nusu saa.Saa mbili usiku nikapaki chuma Moro.