Tupe maoni yako kuhusu amri ya mahakama ya kubomoa gorofa 12 za lile jengo karibu na ikulu

KITEKSORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
346
Reaction score
425
Ndugu wanaJF nimesoma katika magazeti ya jana na leo kuhusu amri iliyotolewa na mahakama kwamba gorofa 12 kati ya 18 za jengo lile lililojengwa pale karibu na ikulu zibomolewe! Hii kitu inasikitisha sana.

Eti jengo lile linahatarisha usalama wa ikulu, sasa najiuliza wakati linajengwa huo usalama wa ikulu haukuwa muhimu?

Wahusika wa usalama wa ikulu hawakuona ujenzi huo? Je kwa technolojia ilivyo juu sasa mtu ni mpaka aje asimame juu ya gorofa kutungua ikulu? Na je kulibomoa sasa ina tija yoyote kwa nchi masikini kama hii?

Mimi nadhani uamuzi huu utafanya watanzania tuonekane kama manyani mbelele ya jamii ya kimataifa. Sasa basi angalau serikali iamue kulichukuwa badala ya kulibomoa.

Lichukuliwe likabidhiwe kwa JWTZ au Wizara ya Mambo ya ndani! Serikali ilichukue ilitumie ila tu ulinzi uwe wa hali ya juu pasiwe mahali pa kuingia hovyo hovyo!

Wewe kwa hekima na busara zako una maoni gani ndugu yangu kuhusu hili jambo?
 
Mleta mada hapo mwishoni umetoa maoni yenye tija sana. Ni hasara ya hali ya juu kulishusha ghorofa lenye hadhi nzuri kama lile (Royal Palm Plaza) naunga mkono hoja yako.
 
Mi nasapoti serikali ichukue zile ghorofa 12 lakini labda mwenye jengo si swahiba wa viongozi wetu maana uswahiba ndo kila kitu watu hawalipi kodi kisa uswahiba!
 
Mm naona jengo libaki
Ninapendekeza ni tofauti
Kwanza sioni sababu ya ikulu kuwepo maeneo ya katikat ya mji km vile
Kiusalama pale ilipo sio pazuri hata kidogo
Watafute maeneo ya nje ya mji na sio lazima tujue ikulu ni wapi lkn iwe nje ya mji
Hii itasaidia vitu vingi ikiwepo kupunguza misafara isiyo ya lazima na kupunguza foleni mjini
Ikulu ya sasa iwe ni makumbusho tu utawala wa kikoloni
 
Kwani mwenye jengo wakati akijenga alipewa stop order akakaidi? kama alipwewa building permit kosa lake nini?
Kisha mimi naoma kubomoa ni uharibifu wa mali ambayo tayari imeshakuwa na thamani.

kimtazamo wangu Kubomoa ni ujinga.
 
Mi naona hili jengo kwanza ni zuri sana linapendezesha mji.cha msingi serikali ikubaliane kuweka tu ulinzi wa hali ya juu.au hizo ghorofa 12 zichukuliwe na serikali.
 
Nani alivunje? Hakuna gorofa litavunjwa hii ni movie mpya ua mwaka huu. Ikvunjwa walahy natembea uchi kilometa 10
 
Jengo livunjwe, kwani athari za kuliacha ni kubwa kuliko jengo kubaki. Nchi yeyote hujiandaa kiusalama katika hali zote, mkiwa hamna adui na kama mkiwa na adui.

1) Kuna ambao mnapendekeza kuwa ghorofa za juu, zichukuliwe na UWT,
Hili si busara, kwa sababu kuu mbili
a) Hapo itakuwa soft tarrget, kama kuwaweka vijana wetu chambo iwapo jasusi anataka kulipa kisasi, kwani itakuwa ni kazi kubwa saana kumiliki na kujua nani wanaingia kwenye jengo hilo, ni rahisi saana mwanya kutokea, hayo makosa hatutakiwi kuyapa nafasi.
b) Pia ni rahisi mwenye jengo, kutumikla mataifa ya nje kutaka kujua na ku monitor mwenendo wa vuijana wetu wanaokaa hapo, na hata kuweka vyombo vya mawasiliano ambavyo vinaweza kujua mienendo na mawasiliano ya vijana wetu.
c) Kma tukipata ugeni mkubwa kama uliopita, hawa jamaa wataomba kukaa na katika jengo hilo kwa usalama wa kiongozi wao, na wao ki maadili watataka kujua ni nani wanakaa kwenye jengo hilo na wataweka vyombo vyao, na hapo tutatoa nafsi kubwa saana kujua idara yetu na hiyo ni hatari saana kwa kwa taasisi yetu.

2) Waopendekeza lichukuliwe na JWTZ, mahali lilipo na palivyokaa, si busara na kitaalamu kuweka vyombo vikuu karibu kiasi kile , maadau wanaweza kutumikla katika kutuadhibu kirahisi saana, kwanza mtu akaamua kulishusha hapo, impact yake hata ikulu itayumba.

Ni bora tulishushe, athari zake ni kubwa, lazima tuwe tayari hata kwa wakati tusio ujua.

Niishie hapa kwa leo
 
aiseeee babayangu mi nadhani mwenye jengo alilikatia bima jengo lake wakati anajenga so atalipwa mara 3 ya garama alizojenga
 
Hapana Hebu busara itumike jaman either serikal ilinunue lote au wapangishe usalama wa taifa gorofa ya Saba na kuendelea kwa sababu naiman Hata lilipokua linajengwa......mkulu alikua anafurahia kuona urefu wake....
Au Hilo nalo alisubir ashauriwe na washaur.wake.kua.ili jengo n hatar??
 
 
Ipeni sheria matwakwa yake, achaneni na porojo wala kutafuta huruma ya jamii, mlichagua kutumia hela zenu kwa njia ya hatari namna ile, sasa hatari inatokezea for real mkabiliane nayo (jiandaeni kutundikiwa madrip ya maji hospital)

kufumbia macho sheria kumetumalizia tembo wetu. SHITUKENI
 

sheria hailihitaji jengo refu liwepo pale, kwa maana hiyo liondoke haraka iwezekanavyo. msilete fikra chanya kuzipakia kwenye gari bovu.

manake hapo ni sawa kuandaa biriani nzuuuuri lakini nyama uliyotumia ikawa ya nguruwe!!
astaghfulilah! astaghfulilah!
 
Wapeleke ikulu Dodoma kwa nini wang'ang'ania dar...kule maeneo makubwa tu kibao wahame sasa mji usijengwe basi ili ibakie ikulu tuu... Dar wabaki wafanyabiashra tuuu
 
Naona Libomolewe Tu, mahakama Imeshaamua.
Nashangaa Mahakama Kwanin Hajatoa Siku Liwe Limeshapungunguzwa. Hatutaki Mambo Ya Kubebana.
Unataka Wapewe Watu Fulani Je Sheria Haitakuwa Imefunjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…