Ndugu wanaJF nimesoma katika magazeti ya jana na leo kuhusu amri iliyotolewa na mahakama kwamba gorofa 12 kati ya 18 za jengo lile lililojengwa pale karibu na ikulu zibomolewe! Hii kitu inasikitisha sana.
Eti jengo lile linahatarisha usalama wa ikulu, sasa najiuliza wakati linajengwa huo usalama wa ikulu haukuwa muhimu?
Wahusika wa usalama wa ikulu hawakuona ujenzi huo? Je kwa technolojia ilivyo juu sasa mtu ni mpaka aje asimame juu ya gorofa kutungua ikulu? Na je kulibomoa sasa ina tija yoyote kwa nchi masikini kama hii?
Mimi nadhani uamuzi huu utafanya watanzania tuonekane kama manyani mbelele ya jamii ya kimataifa. Sasa basi angalau serikali iamue kulichukuwa badala ya kulibomoa.
Lichukuliwe likabidhiwe kwa JWTZ au Wizara ya Mambo ya ndani! Serikali ilichukue ilitumie ila tu ulinzi uwe wa hali ya juu pasiwe mahali pa kuingia hovyo hovyo!
Wewe kwa hekima na busara zako una maoni gani ndugu yangu kuhusu hili jambo?