Tupe maoni yako kuhusu amri ya mahakama ya kubomoa gorofa 12 za lile jengo karibu na ikulu

Tupe maoni yako kuhusu amri ya mahakama ya kubomoa gorofa 12 za lile jengo karibu na ikulu

Nafikiri tuna tatizo la weledi kwa watu wetu wa usalama.Hivi kweli kwa technology ya sasa inahitaji adui kupanda ghorofa ili haidhuru Ikulu? Sasa hivi adui anaweza kuweka on target miji mikubwa ya Marekani akiwa Seoul Korea bila kusafiri.Labda mniabie ulinzi wetu wa zamani, wa kurusha mawe.Ninachoweza kushauri kama jengo limekiuka utaratibu kwa kuongeza ghorofa basi ziitaifishwe,period.Mambo eti ya usalama ni nonsense.Kama serikali wanaogopa basi hilo jengo liwe restricted,ziwekwe detector machine na kamera chini unapoingia kwenye jengo hilo.Gharama itapungua kuliko kupunguza ghorofa.
 
Why ikulu hisiamishwe maana mpaka hapo ikulu yetu ipo ufukweni na hapo sio salama kabisa mara mia ya hilo gorofa kuwepo hapo
 
Me naona serikali imlipe fidia mmiliki wa jengo kwa ghorofa sita za mwanzo halafu hizo zingine wapewe vitengo vya usalama kama TISS,TPDF,na makao makuu ya polisi yahamishiwe pale
 
Mi naona jengo ilo mwenyewe apewe fidia Kisha litumiwe na idara za usalama nchini ila kulibomoa tu ni kurudisha maendeleo nyuma.
 
Sheria inasema kuna idadi ya ghorofa zinazostahili kujengwa eneo lile hata kama ni jengo la wizara. Hivyo hata serikali kulichukua jengo hilo itakuwa ni kuvunja sheria. Kama kweli tunatekeleza utawala wa kisheria basi itabidi hukumu ya mahakama itekelezwe!

Siamini iama kweli litabomolewa.
 
Ndugu wanaJF nimesoma katika magazeti ya jana na leo kuhusu amri iliyotolewa na mahakama kwamba gorofa 12 kati ya 18 za jengo lile lililojengwa pale karibu na ikulu zibomolewe! Hii kitu inasikitisha sana.

Eti jengo lile linahatarisha usalama wa ikulu, sasa najiuliza wakati linajengwa huo usalama wa ikulu haukuwa muhimu?

Wahusika wa usalama wa ikulu hawakuona ujenzi huo? Je kwa technolojia ilivyo juu sasa mtu ni mpaka aje asimame juu ya gorofa kutungua ikulu? Na je kulibomoa sasa ina tija yoyote kwa nchi masikini kama hii?

Mimi nadhani uamuzi huu utafanya watanzania tuonekane kama manyani mbelele ya jamii ya kimataifa. Sasa basi angalau serikali iamue kulichukuwa badala ya kulibomoa.

Lichukuliwe likabidhiwe kwa JWTZ au Wizara ya Mambo ya ndani! Serikali ilichukue ilitumie ila tu ulinzi uwe wa hali ya juu pasiwe mahali pa kuingia hovyo hovyo!

Wewe kwa hekima na busara zako una maoni gani ndugu yangu kuhusu hili jambo?

jengo libaki ikulu iende dodoma...afu napingana na ww kusema eti jengo lichukuliwe na JWTZ au usalama kwani wanaopinduaga nchi c no hao hao ikulu iende dodoma na wizara zote ziende huko dar tuache biashara
 
Sheria inasema kuna idadi ya ghorofa zinazostahili kujengwa eneo lile hata kama ni jengo la wizara. Hivyo hata serikali kulichukua jengo hilo itakuwa ni kuvunja sheria. Kama kweli tunatekeleza utawala wa kisheria basi itabidi hukumu ya mahakama itekelezwe!

Siamini iama kweli litabomolewa.
Mkuu hizo sheria wakati hilo jengo linajengwa mpaka kufikia hapo lilipo zilikuwa likizo? Jengo halijengwi siku moja linakwenda kwa hatua ambazo nina hakika ziliridhiwa na serikali kwa njia ya vibali mbali mbali. Iweje leo lionekane linahatarisha usalama wa ikulu?
 
Tupe maoni yako kuhusu amri ya mahakama ya kubomoa gorofa 12 za lile jengo karibu na Ikulu.

Mimi ninakubaliaa na hukumu ya mahakama. Nakiri hivyo kwa kuwa imethibtika bila shaka yeyote kwamba maofisa wa serikali wliopaswa kusimamia sheria kuhusu ujenzi wa eneo hilo walikiuka taratibu zao za kazi. Hukumu hii imeweka historia kwa watu wengine wenye nia ya kutumia fedha kufaniksha matakwa yao kiuchumi au vinginevyo. Serikali kulichukua tuu kwasababu ya ukiukwaji wa sheria haitakidhi matakwa ya usalama uliokua umekusudiwa na serikali. Kwa kuchukuliwa na Jeshi si salama bado. Ingekua Jeshini ni salama, ikulu ingejengwa kweye mojawap yakambi za jeshi.
Mimi nakubaliana na uamuzi wa mahakama asilimiamoja. Kutokujua sheria si kinga ya kusamehewa kosa.
 
Back
Top Bottom