Phone4Sale Tupe maoni yako

TECNO Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
192
Reaction score
217
Habari Ndugu!

Ikiwa tume uwanza mwaka mpya basi nasi tunataka tukuhudumie kwa viwango vya juu kabisa kwa mwaka huu kwa kuwaletea matoleo mazuri zaidi na ya kisasa.

Leo tujadiliane kitu kimoja. Kwa namna moja ama nyingine simu zetu za TECNO zimekuwa na watumiaji wengi sana hapa nchini. Huku ikionesha kuwa asilimia kubwa ya watanzania hupendelea na huvutia wa na sifa tofauti tofauti pale wanapotaka kununua simu.

Je wewe ukiwa kama mtumiaji wa simu janja ni sifa gani zaidi zinakuvutia unapotaka kununua simu mpya ni Camera, Battery kubwa, Storage kubwa, Design, Price au Processor.



Kwa mawasiliano na taarifa zaidi piga simu namba 0744 545 254 au 0678 035 208.
 
Pamoja na kioo kizuri, nguvu ya simu mimi navutiwa na teknolojia mpya. Napenda sana sana Simu yangu inapo switch kwenda kwenye vibration automatic pindi nnapokua kazini na kurudi kwenye mlio nnapokua nyumbani na barabarani. Hivyo hivyo kuwasha wi-fi automatic pale nnapofika sehemu zenye wifi nnazo tumia mara kwa mara. Pia napenda performance ya uhakika na network syable hasa ninapocheza game langu pendwa Pubg sipendi kuona simu inastack kwani itaniweka kwenye competitive disadvantage.
 
Msikimbilie kutoa matoleo mapya kwa muonekano wa nje wakati ndani hakuna kipya
 
Mkuu, sorry naomba kujua.... hivi hakunaga option ya ku set vibration and vice versa kama vile tunavyo set alarm!?
 

Asante sana Boss kwa maoni yako. Tutahakikisha tunalifanyia kazi
 
Mkuu, sorry naomba kujua.... hivi hakunaga option ya ku set vibration and vice versa kama vile tunavyo set alarm!?
Hapana sio Alarm ni smart nikifika maeneo ya kazini inadetect inaweka vibration only nikitoka tu inarudi kwenye mlio. Hata kama ni mara 10 kwa siku.
 
Tecno kama tecno au sio. Mimi naonaga mnabadili miundo ya juu tu mara kamera ikae huku na kule ila ukichunguza ndani mzigo ule ule sjui mnakwama wapi. Alafu unaweza kuta tecno ina specification za maana ila huwezi fanyia kazi za serikali kiufupi ukiwa na app 2 tu za serikali simu inaanza kustack japo ina uwezo mkubwa hili nalo mkalitazame. Alafu mje na jina jingine asee hizi sisi tushaziona kama redio tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…