Tupeane elimu ya macho katika ulimwengu huu wa Kidigitali

Tupeane elimu ya macho katika ulimwengu huu wa Kidigitali

renamaizo

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
2,134
Reaction score
3,064
Habar wakuu,

Nadhani sisi wote tunatumia digital devices lakini shida ya hivi vifaa vinasababisha matatizo ya macho lakini ajabu ni kwamba wapo watu wameajiriwa kama secretary au developers muda mwingi wapo on screen na hawana miwani au matatizo ya macho, sasa najiuliza hawa wanawezaje?

MASWALI YANGU NI HAYA
1. Chanzo cha matatizo ya macho ni mwanga au nikuangalia vitu vya karibu?

2. Je, ni eneo gani la jicho huathirika baada ya kutumia digital device lens, retina au nini?

3. Je, mwanga mkali na mwanga hafifu upi unaumiza macho?

4. Je, mwanga wa jua unaweza kukuathiri pia?

Mimi yangu hayo tu mengine wadau ongezeeni tupeane tips zilizoenda shule madaktari pia mnakaribishwa.
 
Mimi nilipata myopic astigmatism
Yani jicho moja linakua halioni mbali.

Nilipata hii ishu baada ya kuwa nashinda sometimes usiku kucha nasoma kwenye computer, yani sometimes asubuhu hadi asubuhi naweza kua on screen ni kusoma na kucheza games tuu.. nikipata off ni wakati wa kula tu 😄
Ishu ilikua worse baada ya kila siku kuwa on bike takriban km 10 wakati wa mchana nikitoka mishe, jua lilikua linaniumiza sana hadi kazini wakanishauri nikafanye eyes check up sabab waliona nilivokua na "severe eye strain" ingawa mimi nilikua sijijui.
Condition ikawa worse nikawa napata maumivu ya kichwa mara kwa mara na pia nilikua napata mazigazi "aura" kwa sana, then nikaanza kupata kichefuchefu ndipo nikakubali kupima nikakutwa na ishu hiyo..

So now ni nwaka na miezi kadhaa navaa miwani tu..
Ishu inaonekana haitapona sababu nikitoa miwani baada ya masaa kadhaa naanza kuwashwa nyusi, ila nikivaa tu hali hiyo inapotea.
My take; Kama ni mtu wa kushinda juani au kwenye screen basi nenda kafanye eye check up then wakupe ushauri miwani gan uitumie ili ujikinge na haya majanga

Kinga ni bora kuliko tiba ✊
 
Back
Top Bottom