Tupeane maujanja ya Excel

Mkuu hapo kuna function inaitwa COUNTIF nakuandalia maelezo mafupi Kwenye clip
UKo sawa mkuu, ila mi nilifikiria kutumia filter ... ila countif ndo inapiga penyewe
 
home>> Review>> Protect Sheet

Hapo utaweza kuifunga sheet yako mtu mwingine yeyote asi edit au kupunguza kitu unaweza ukaweka password lakini inatakiwa uwe makini kwasababu ukiisahau haiwezi kurudishwa....
Hapo hapo mkuu mm nataka kuprotect formula mtu mwingine asibadili but awe na accses ya kubadili data tu. Nafanyaje hapo mkuu?
 
Uzi upo kimya kinoma yaani na.kule Telegram ndo naamini majukumu nayo yanachangia ila jitahidi mkuu kwa hilo maan nahitaji msaada kuhusu hii kitu ya pivot table nimejaribu fatilia tutorial videos youtube ila nimetoka kapa nime google wapi samahani mkuu sjui unaweza nisaidiaje lengo nahitaji kufahamu pivot table inahusu nn zaidi,inatumikaje,na jinsi ya kuandaa mkuu maan nmeona ni njia flani ambayo ina rahisisha kazi sana ila sjaelewa kiundan so bado nashauku ya kupata elimu juu ya hii ko mkuu Ethos au yeyote mwenye ufahamu naomba msaada.ahsanteh!
 
Ziweke alama column ya kwanza kwa majina yote, highlight majina yote na marks zake, light click then select Sort A-Z, ngoma itakupangia flesh
Select majina cell zote kasoro s/n nenda sort and filter utakuta custom sort chagua column ya total na largest to smallest then drag
 
Nalitambua hilo mkuu.. Nilikua safarini kidogo hivyo muda wa kukaa kuandaa video fupi umekua finyu... Pardon my lateness
 
Hapo hapo mkuu mm nataka kuprotect formula mtu mwingine asibadili but awe na accses ya kubadili data tu. Nafanyaje hapo mkuu?
Kama sikosei ukishaprotect cell, kilichopo kwenye hiyo cell ndo kinakuwa protected. Unajua how to protect cell?
 

MAELEZO HAYA YANAELEWEKA AU?
A PivotTable report is an interactive way to quickly summarize large amounts of data. Use a PivotTable report to analyze numerical data in depth and to answer unanticipated questions about your data. A PivotTable report is especially designed for:

  • Querying large amounts of data in many user-friendly ways.
  • Subtotaling and aggregating numeric data, summarizing data by categories and subcategories, and creating custom calculations and formulas.
  • Expanding and collapsing levels of data to focus your results, and drilling down to details from the summary data for areas of interest.
  • Moving rows to column or columns to rows (or "pivoting") to see different summaries of the source data.
  • Filtering, sorting, grouping, and conditionally formatting the most useful and interesting subset of data to enable you to focus on the information that you want.
  • Presenting concise, attractive, and annotated online or printed reports.
You often use a PivotTable report when you want to analyze related totals, especially when you have a long list of figures to sum and you want to compare several facts about each figure. In the PivotTable report illustrated below, you can easily see how the third-quarter golf sales in cell F3 compare to sales for another sport, or quarter, or to the total sales.

Baada ya majibu nitaweka mfano rais tu ili uweze kujua kinachoongelewa ... soma kwanza ...
 
Pivot table inasaidia ku-summarise information iliyoandaliwa kwenye Ms Excel.
Mfano unafanya mauzo kwenye duka na kila kitu unakiandika kama kilivyo. Kuna items zitajirudia mara kwa mara kwa siku tofauti tofauti. Utakapohitaji kufocus kwenye specific item / product ndo itakubidi utumie pivot table kwa kuwa makini na nyanja zifuatazo:-
Report filter
Column lebels
Row lebels
na Value
Kama umenielewa vyema sema tuanze kupeana mifanyo hapa hapa.
 
Kama sikosei ukishaprotect cell, kilichopo kwenye hiyo cell ndo kinakuwa protected. Unajua how to protect cell?
Hapana mm najus tu kuprotect the whole sheet. Hebu nielekeze hyo ya kuprotect sheet
 

Nimekuelewa nilikuwa offline kidgo kwa sku mbili ndo maana nilikuwa kimya so tunaweza endelea mkuu
 
Naomba kujulishwa jinsi ya kuandaa matokeo ya mtihani, jinsi ya kuwapanga wa mwanzo hadi mwisho kwa kuzingatia column ya JUMLA bila kuathiri mpangilio wa alama za masomo kwa kila somo.
Njia mzuri zaidi ni kuhighlight data zote (mwanafunzi wa kwanza hadi wa mwisho) kisha click sort, chagua customize sort, litakuja dialogue box, chagua column unayotaka kusort(jumla) kisha chagua aina ya sort (A-Z au Z-A) na bonyeza ok. that is all guys.
 
Mkuu msaada tutani lengo langu niwe na kitabu kimoja cha debtors kwenye biashara yangu nime shameshawafungulia kila mmoja acc yake sasa nataka niwe na debtors summary yaani badala ya kuangalia mmoja mmoja niwe naupdate acc zao afu change zitokee moja kwa moja kwenye summary tu kila mmoja anadaiwa sh ngap, sasa nashindwa weka formula mkuu inanipa shida kidogo
 
Ebana mi kwa kazi yangu nahitaji kujua ile sijui pivot table..... yaani inanirahisishia sana kufanya kazi zangu. Ninafanya Simple accounting, Table yangu ina Date, Description, Department, na Amount. Sasa nnachotaka mimi yaani hio Pivot sijui inioneshe summery ya kila department na date zake, only summery, Table ya kawaida ndo itaonesha all details, hii ya pivot ioneshe total amount ya each date on each department
 
Unatumia Ms excel au? Ebu weka hilo file lako alafu upatiwe ufafanuzi haraka haraka ...
 
Weka fields / columns ulizonazo kwenye hiyo table yako then uweke sample names let say 20 debtors - utaelekezwa vyema tu!
 
Hapana mm najus tu kuprotect the whole sheet. Hebu nielekeze hyo ya kuprotect sheet
Ebu kuwa wazi .. unayajua haya vizuri
Workbook = hili ndo file lilisaviwa kwenye excel
Worksheet = sehemu ya kufanyia kazi
Column = mgawanyo wa wima
Row = mgawanyo wa mlalo
Cell = Mahali zinapokutana column na row
Usichojua kuprotect ni kipi kati ya hayo yote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…