Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.
Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.
Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?
Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?
Tushirikiane kupeana mawazo wandugu
Maty mpendwa kuna mambo hayavumiliki , me wifi yangu hadi alitaka kufa na ujauzito kwa pressure mume ana nyumba ndogo 3 na zote ni wadada wa mujini na familia ya kiume inajua, mume anarudi manane ya usiku hadi apige round nyumba ndogo zote. Wazaz wanamwambia avumilie. Hamjali kamtelekeza na mtoto wa miaka 4. Hapo kuna uvumilivu tena???
Nnunu nimeshaingia kazini. Nachoweza kusema kuhusu nyumba ndogo si kuwa inarekebisha nyumba kubwa ila inafanya husband arudie vows. Maana nikigundua kuna kimada mziki wake ni lazima urudie maneno yote mazuri ulonambia toka tuna date mpaka unaapa kanisani. Haa. Mwanzo wife anakuwa na hasira, baada ya muda anashukuru nyumba ndogo kwani amefufua mapenzi katika ndoa. Kwa experience yangu wanaume wakibambwa wanarudisha descipline na mapenzi yana double! Na hii si kurekebisha nyumba kubwa ila inamfanya mume nae atie akili. Unafikiri ni rahisi ku divorce mke alokuzalia watoto wanaokufanya nawe uitwe kidume.
Mimi nina experience ya ndugu yangu yaani mume wake alicheat alafu yeye mwenyewe cheater ndo kaita kikao cha wana familia kwani anaogopa ndoa isije vunjika.
Inawezekana mkikaa bila hawa vicheche ku interrupt ndoa yenu ndoa ikawa boring. Hizo ndo challenges zenyewe. Ila sasa kilichoharibu maradhi!
Mi mwenzangu najivumilia tu milima mabonde mafuriko elninyo nimo tu, mbele kwa mbele huko tutajua
ndoa za Dot.Com ni ngumu kuzihandle, tuvumilie tu!
degree ya uvumilivu kwenye ndoa ni ndogo sana kwa maisha ya sasa
ukizingatia wana ndoa wengi wana'jua' haki zao na hakuna anayetaka kujiweka chini
haya yote nadhani yameletwa na utandawazi..na hii kitu equality wanawake tunaililia pia i think inachangia kwa namna moja au nyingine
hakuna mwanamke wa siku hizi anataka kunyenyekea, wote wana/tuna penda kujilinganisha na wanaume..
mbaya zaidi ukikuta mdada kasoma ndo kabisaa hapo ni maswala ya 'nini nini usinichoshe nisikuchoshe nataka amani'..
tofauti na mama zetu walikuwa ni wanyenyekevu wazuri sana na wao pia walikuwa wanaangalia consequences za kuachana kwa watoto
lifestyle imebadilika generation hii ni selfish haiangalii watoto
in a nutshell, anayeweza kuifanya ndoa iendelee kuwepo ni mwanamke, na mwanamke wa sasa si mvumilivu.
Ni mtazamo tu.
nilidhani lbd ndoa za kilokole zinaweza kuwa na unafuu!!
Hivi juzi tu hata mwezi haujaisha dada mmoja mpiganaji kweli kweli na mwanamaombi aliolewa na kk mmoja mlokole mwenzie, kweli harusi ilikuwa nzuri!! wiki ile niliyofiwa akaja kunipa pole akiwa na mama mmoja mchungaji rafiki yangu, baada ya kuona muda umeenda sana, nilimuuliza nawewe unakesha?? akasema ndio, nikamuuliza shemeji vipi hata kasirika akasema tumeshaachana!! nilishika mdomo.
kumbe nasikia walitengana baada ya week 2 tu!! yule mama mchungaji aliniambia kuwa baada ya tu ya siku 2 za ndoa akaanza kusuluhisha kesi zao mpaka mwisho amechoka.
Nikasema duh!! kwakweli kuna haja ya kuendelea kuwa single mpaka kieleweke!!!
mimi yalinikuta na naapa sitakaa nioe tena hapa duniani,nina 40years old,wanawake wakiwa na kazi na pesa wanakuwa na kiburi ambacho hakuna mwanaume wa kuzuia,na kama unaona mwanamke mwenye pesa anaishi kwenye lindoa la matatizo ujue hapo kuna kitu,labda huyo mwanamama ana kahuruma na watoto,thats all,dunia inabadilika na hii ndio hali halisi:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
Usiogope mwali doa zote sio lazima ziwe na matatizo, ila ujue pia kila siku sio jumapili. jiweke imara ili hata kama yakikupata matatizo ujue unakabiliana nayo vipi. Meanwhile enjoy you marriageThe topic is hot...Ndoa yangu bado changa so naobserve na kulearn... Thanx Maty kwa kuanzisha hii thread... Okey, 2endelee...
ha ha ahaha nimecheka mpaka machozi ya furaha yamenitoka, ASANTE KWA KUNIONGEZEA UHAI NA AFYA YANGU,,,kumbe sikukosea kukumiss kwenye hii thread nzuri ya MATY....yaani napiga picha kama nakuona unavyojifanya umekasirika sana,kumbe nia yako mume aendelee kukubembeleza zaidi....kubebembelezwa kuna raha bwana asikwambie mtu....na hasa ukibembelezwa na kiumbe kinaitwa mwanaume, raha yake haisimuliki ilivyo nzuri....safi sana nyumba kubwa umeonesha ni jinsi gani unaujua utamu wa kubembelezwa na mume.....lol
Dah! mawazo yenu niliyoyapata hapa inaonyesha ndoa ni ngumu sana asee