Hongera sana kwa kufikiria wazo la kufanya biashara. Ila biashara yoyote ya chakula na nyenginezo nguzo kuu ni moja.
1. Location
2. Location
3. Location
Eneo kijana katika biashara ambayo inakupa jibu ndani yasiku moja imezidi mbili yakuwa umepata hasara au faida ni biashara ya butcher. Wekeza mda wako mwingi kutafuta eneo stahiki utafanikiwa lakini kama ukikosa eneo stahiki usidhubutu kufanya hii biashara maana. Utapata tu hasara na kutupa fedha zako.
Jiandae na msingi usiopungua milioni 7 hivi.
1. Mashine ya nyama inatembea 2,200,000 - 1,800,000 achana na zile za kitonga.
2. Frem eneo kidogo potential jiandae 200,000 mpaka 400,000 per monthly
3. Meza ya aluminium around 250,000 mpaka 500,000
4. Zile chuma zakuning'iza andaa 500,000 - 300,000
5. Gogo la emergency 80,000 - 40,000
6. Shoka, Visu , nguo , Gambuti, havizidi 100,000
7. Mlango wa alluminium 600,000 - 380,000 inategemea na vipimo vya frem yako
8. Friza jipya usinunue used 700,000
9. Tiles andaa 1,000,000 - 800,000
10. Leseni 80,000 Tra tegemea makadirio 800,000 - 250,000
11. Chakushangaza msingi wa nyama 330,000 kwa bei ya machinjioni 8,000 maximum kg 40 na gharama zakufika ofisini kwako.
Kwa makadiro hayo hilo ni bucher standard likiwa chini ya hapo msingi unaweza pungua.
Tahadhari.
1. Eneo
Hakikisha unafungua butcher sehemu yenye mzunguko na uhitaji wa nyama kwa wateja kama Sokoni, Stendi au sehemu ambayo unajua kwenye uhitaji. Angalia bar zipo karibu, mama ntilie, Wauza chipsi maana hawa nao niwateja wako. Sasa ww chinjanganye uchague sehemu sio hiyo milioni 7 sjui 6 itapotea yote alafu hutojua ilipopotea[emoji2][emoji28][emoji24]
2. Muuzaji
Hakikisha unakuwa na mtu dhamana sana atakae kuuzia nyama na mzoefu huyu ndo atakae fanikisha lengo lako usiokote mtu humjui wengi hukimbia na mitaji, wanahonga, wanakuibia na biashara hii imetawaliwa na ndugu zetu wa Dodoma kuwa makini nao. sasa ww weka dharau hili hutoacha kuona rangi zote na utaichukia hiyo biashara.
3. Ushirikina
Hakikisha usifungue hii biashara kama hujajipanga utajua mwenyewe vya kufanya kumbuka hiyo ni damu [emoji28][emoji3][emoji24]. Kuna wale wazee wachuma ulete na mengineyo
4. Msingi wa nyama
Hakikisha unakuwa na msingi wa nyama miwili yaani back up huu ukiyumba kidogo unakuja na back up nyengine.
5. Faida na hasara
Faida ya nyama ni 2,000 au 1,000 kwa kg ndomana nikakwambia akili yako iwe kwenye eneo unavoo uza ndofaida inapoptatikana
Mfano umeuza kg 40 faida 78,000 kuna kg inapotea sasa hiyo 78,000 utamlipa muuzaji 10,000, Msosi juu yako na gharama za kusafirisha nyama kutoka machinjioni kuja kwako weka 10,000 na msosi 10,000 sjui taka na mengineyo utabaki kama na 40,000.
La Mwisho
Jitahidi ununue mwenyewe machinjioni au uwe na supply maalum hapa ndo kwenye shida ya kuamka alfajiri inahitaji moyo sana ila ukikaza kiume utafanikiwa na hapa ndo msingi wa biashara yako usicheze kabisa kuna siku soko linaanguka huko machinjioni bei zinashuka unapiga hela vibaya ukija kuleta ofisini kwako.
Mfano biashara kwao ikiyumba baada ya kununua 8,000 unawalalia ukanunua hata 6,000 bonge la faida kwako unakuja kuuza 10,000 ofisini kwako sasa 4,000 × 40 bei gani aisee.
Kila la gheri mkuu