Tupeane updates kuhusu mikopo ya Mabenki

Tupeane updates kuhusu mikopo ya Mabenki

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Habari waungwana wa jf.

Taarifa nying kuhusu mikopo kutoka Taasisi za kifedha nchini ( Bank) ni za muda Sana.

Binafsi nafikiria kwenda kuomba mkopo CRDB au NMB.

Naomba maoni kutoka kwenu wadau juu ya Mambo Kama.
1. Riba.
2. Masharti.
3. Ubora wa huduma n.k

Mkopo ninaoomba dhamana yake ni mshahara wangu kutoka Hazina ( mtumishi wa Umma)

Naomba kuwasilisha.
 
Kila la kheri. Na hongera in advance kama utaweza kuchomoka baada ya kuingia huko. Ila pole in advanve pia mkopo ukienda ndivyo sivyo. Yakwangu ni hayo
 
Kopa kwajili ya mambo ya msingi narudia tena yale yamsingi au ya uwekezaji.

Pia mkopo usiwe wa muda mrefu sana mitatu mwisho.

Za kuambiwa changanya nazako.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ungetushirikisha na plan yako pia ili iwe rahisi kukushauri...mkopo wa kiasi gani na kwa muda gani?
 
Soma kuna uzi upo humu

Wa waliochukua mikopo wakaitumia ndivyo sivyo
 
Mi ushauri wangu chukua mkopo usizidi miaka miwili.Asante.
 
Dogo print salary slip yako kisha panga kiasi unachotaka kukopa kisha tembelea benki unazohisi unataka kukopa watakupa every details then unafanya maamuzi hapa hakuna majibu,

Suala la riba linategemeana na muda wa mkopo na kiasi
 
Kila la kheri. Na hongera in advance kama utaweza kuchomoka baada ya kuingia huko. Ila pole in advanve pia mkopo ukienda ndivyo sivyo. Yakwangu ni hayo
Kuchomoka kwenye mikopo ya bank ni jambo gumu sana....linahitaji mkakati wa kweli
 
Kuchomoka kwenye mikopo ya bank ni jambo gumu sana....linahitaji mkakati wa kweli
Inawezekana Sana mkuu, Mimi nimechukua mwezi wa tatu CRDB 11milion mwezi wa Saba naenda kuwalipa hela yao yote tufunguane mashati. Japo inahitaji kuvaa mabomu kwa hali ya juu Sana.
 
Inawezekana Sana mkuu, Mimi nimechukua mwezi wa tatu CRDB 11milion mwezi wa Saba naenda kuwalipa hela yao yote tufunguane mashati. Japo inahitaji kuvaa mabomu kwa hali ya juu Sana.
Tusaidie ulifanya biashara gani??.
 
Back
Top Bottom