Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

Hivi Gwaride huwa ni wote mnapiga kila siku au? na kwenye zile shughuli maalumu mfano za kuhitimu huwa wanachagua wakupiga Gwaride au wote?
 
Jamani nia na madhumuni ya Uzi huu ni kupeana updates mbalimbali Kwa wale tulio omba ajira za jeshi la polisi 2024 kama Kuna yeyote anajua chochote kuhusiana na CCP akuje atupe mwanga, mbinu za kutoboa pamoja na life la huko

Asantni🙏
Mbinu ni moja tu. KADI YA UVCCM.
Hii utaivaa shingoni kama ID uingiapo kwa interview. Hautoulizwa chochote utajitambulisha tu na utakua umemaliza kila kitu.
 
Hivi Gwaride huwa ni wote mnapiga kila siku au? na kwenye zile shughuli maalumu mfano za kuhitimu huwa wanachagua wakupiga Gwaride au wote?
HAPANA,kule kuna Kombania,mfano Kombania A,B,C na Headquarter,na kila Kombania inajitegemea kwenye kulala kuna mabweni yao,kula kila Kombania ina Mess na Jiko lake,Maafande wake nk.Hivyo hata kufoleni mnafoleni kwa Kombania. Kwenye gwaride kunakuwa na mgawanyo kwa maana ya kwamba kuna ratiba. Wengine wanaweza kuwa darasani wanasoma vipindi,wengine wapo paredi wanapiga kwata nk.Kikubwa ni kwamba Mafunzo yote yanakuwa yanafafana kwa kila kombania. Kwenye gwaride la kumaliza ni wote japo wengine wanaweza wakawa kwenye kitengo cha Mafunzo ya Judo na Karate kwa ajili ya kuonyesha show siku ya kumaliza Mafunzo hivyo hao hawatafanya gwaride la kumaliza Mafunzo
 
Shukran sana mkuu🤝🤝
 
Vip na kuhusu utaratibu wa uniform za kuendea kazin…hua wanawashonea mule mule kabla hamjatoka au??…..na je ni kwa size mtu anayotaka au inakuaje…maana kuna askari wengne uniform zao ni bwanga na wengne ni modo
 
Vijana naona ndo wanamalizia kozi wapo kweny semina ukoo, week hii au week ijayo naona PDF litamwagika🔥🔥
Mwezi huu uhakika wanamaliza Depo Maana Walianza Kozi Mwezi Wa 12 Tarehe 1, Muda umefika kabisa...

Wakishamaliza Rasmi Mwezi unaofata wanaungwa kwenye payroll tayari kupokea Mshahara, kwenye picha ni MIHADHARA ya kuwaongezea maarifa katika kazi zao.

Check Number mara nyingi hutoka pamoja na Mshahara wa kwanza.

Issue za Uniform zote mtapewa kule kuanzia vest kaki, Viatu, green jungle, ballet, tt na kadharika... Ila kule askari hupunguza nguo kadri ya size zao ila pia kuna ukaguzi, ukizingua unapewa adhabu ya kutosha.

All the best Kwa Vijana Wanaokaribia Kuhitimu....
 
Nikitoboa nitakuchek inbox kuna vitu nikuulize mkuu
 
Kozi wanafunga October ijumaaa ........psssf tayar wamepewa elimu na kuungwa juz watu wa saccos yao waliend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…