Tupeane updates za matukio ya wizi mitaani

Tupeane updates za matukio ya wizi mitaani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Heshima kwenu wanabodi,

Wakubwa shikamooni,

Ninaleta Uzi huu lengo tuweke wazi matukio ya wizi ambayo yamerudi kwa kasi nchini. Naombeni tuonyeshe jinsi gani wajanja wa mjini wanatuumiza. Imefika kipindi mpaka watu wameuawa kisoosoo. Watu wanaibiwa maduka sio poa.

Okay, kwa kuanza binafsi nataka niwasimulie matukio yalitokea mjini kwetu Singida mtaani kwetu Mwenge na kama wahusika wapo mjue kinachoendelea.

Kwanza nawapongeza jeshi la polisi kwa doria mnazofanya katika mabanda ya kuuza gongo kwa kweli wauza gongo hii week wamekaa kimachale sana wamekaa kindege John kwani hawauzi kama mwanzo licha ya kwamba kipindi Magufuli anahusika na serikali aliwakataza kuwazuia wauza gongo tonge lao mdomoni. Pia na wauza bangi nimeshuhudia wamekamatwa sana.

Matukio ya wizi ni kama ifuatavyo; kuna mtu karakana kaibiwa simu ndani kwake tena mchana, kuna mwingine kaibiwa duka Madera yamechukuliwa yote, kuna mwingine kaibiwa mashine ya kushona, mwingine juzi kaibiwa spares za magari, mwingine kakabwa kaibiwa 30000.

Haya ni baadhi tu jamani mambo yameharibika kiufupi uwizi umezidi kiwango ndugu waziri wa mambo ya ndani tusaidie tutaisha Kama mnaona iko haja msaidiwe na jeshi la JKT au mgambo Basi itakuwa vema.
 
Asee wee jamaa ni ndugu yangu kabisaa!!hapo mwenge nina ndugu kibao sana! Nakumbuka zamani flani alishachomwa moto mwizi hapo, nyuma ya ile sheli.
 
Sisi hapa tarime wafugaji wizi umekomeshwa na hawa askari wa kanda maalum. Shida imekuwa hao askari wa kanda maalum, wanatubambikia sana kesi na kulazimisha tuuze ng'ombe tuyamalize kabla hayajafika kituoni.
 
1581825009257.jpg
 
daahh kweli wee ndugu yangu..
sina kumbukumbu ila ni kitambo sana..
nahisi ni pale kwa meta wale wanauza matofali!!
Me nimesoma mughanga primary nilikua natoka karakana mpk town
 
Me nimesoma mughanga primary nilikua natoka karakana mpk town
Sio mbali of coz labda kwa anaesoma ipembe!mi nimesoma hapo ipembe ila miaka ya 90s, niliondoka mda kipindi hapo karakana hapajawa hata mji.

Nilikuwa nakuja kusalimia tuu baada ya miaka najikuta napotea mitaa tu. Mmungu alijaalia nikajenga vibanda viwili hapo karakana kwa usimamiz wa ndugu ila nilikuwa najutia kujenga nikiona kama ni pori sana, but now nimekubali jinsi watu wameotesha mijengo ndo hivyo kambi popote.

nikija next vacation nakutafuta twende pale ubungo isha NYOKAA au ile club kali pale ubungo jina limenitoka.
 
sio mbali of coz labda kwa anaesoma ipembe!mi nimesoma hapo ipembe ila miaka ya 90s..niliondoka mda kipindi hapo karakana hapajawa hata mji..
nilikuwa nakuja kusalimia tuu baada ya miaka najikuta napotea mitaa tuu..!mungu alijaalia nikajenga vibanda viwili hapo karakana kwa usimamiz wa ndugu..ila nilikuwa najutia kujenga nikiona kama ni pori sana.but now nimekubali jinsi watu wameotesha mijengo..ndo hivyo kambi popote.
nikija next vacation nakutafuta twende pale ubungo isha NYOKAA au ile club kali pale ubungo jina limenitoka.
Rode
 
Nchi hii ni Mali yetu. Usalama wetu ndio amani yetu hapa Duniani. Hatuwezi kuishi na watu wachache mtaani wasiopenda kufanya kazi wakasubiri tufanye kazi wao waje wakwapue na kwenda kukaa viti virefu kuneemeka.

Naamini sisi tunawajua wahalifu ila wao hawatujui. Sisi tunaelewa wanavyotusumbua na wanavyojitamba mtaani lakini hatuna njia ya kuzungumza serikali ikasikia.

Nauweka uzi huu hapa tutupie majiana vijiwe ambavyo ni maficho ya wahalifu lakini pia tuwafichue wahalifu kwa Nick names zao then polisi afanye ufuatiliaji nakuwavua wale watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua.

Tuwafichue tule bata kwa anlmani
 
Sirro alisema kila mwananchi ni wajibu wake kujilinda ,na wananchi lazima tutoe ushirikiano ,naomba kila mwananchi apewe bunduki halafu tuona majambazi wanavamia vipi
 
Back
Top Bottom