Tupeane ushauri namna ya kuwa millionaire kabla miaka 25

Hehe heee

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2017
Posts
213
Reaction score
186
Natumaini muwazima wa afya, nimeandika uzi huu kwa dhumuni la kuwapa motisha vijana na mimi mwenyewe pia kwani katika maisha aya sasa vijana wengi wameamka wakiwa na ndoto kubwa, marengo makubwa, wengine wakitaka kumiliki kampuni zao katika umri mdogo, wengine kuwa mamillionaire katika umri mdogo minapenda kuita (MILLIONAIRE BEFORE 25) hayo yote yanawezekana

Dhumuni la uzi huu ni kutaka kupokea mawazo mtambuka na yaliyoshiba mawazo kuntu kutoka katika kwa ma Great thinker umu jamvini hivyo toa mawazo ukiwa free kabisa kwa dhumuni langu ni uzi huu uwe kama kitabu cha vijana ambao wana mawazo mkubwa ya makampuni na utajiri mkubwa

NB: jiachie vilivyo kwenye kutoka hoja nawasilisha
 
Kitu kikubwa ni self determination na commitment, that's it. Kila mtu ana purpose yake hapa duniani ni kitendo cha kutambua tu lakini bahati mbaya wengi wetu tunaishi maisha yaleyale (usome, ufaulu, upate kazi basi) kwa fikra izo utajiri utaishia kwa wachache tu wanaothubutu kufikira nje ya box ( kama wa kunielewa, umenielewa).
 
Ni ngumu na nirahisi yote yanawezekana chini ya jua Ila Kwa mifumo yetu ni ngumu Sana kama huna mtaji Mkubwa na pia usiwe msomi
 
Waliulize mamilionea. Sasa humu wengi wafanyakazi, wanavyuo na wafanyabiashara ndogondogo ndo wakushauri ndugu? You must be kiding
nikweli kabisa mtu wa maisha ya kawaida au masikini hawezi kukushauri njia za kupata mafanikio makubwa wengi huwa wanahisi tu labda inakuwaga hivi
 
Hapo labda ukaloge au upate mali za urithi kidogo unaweza kuwa millionaire katika umri huo
 
Dollar millionaire au shilingi? Shillingi ukipata kazi yoyote professional ushakuwa millionaire.
Dollar before 25 kwa bongo labda uibe au mtu akupe mtaji mkubwa sana.
 
Milionea ni kumiliki milioni moja na kuendelea. Anza kama ifuatavyo.
Nenda benk nunua kibubu cha chuma funguo waachie na ufungue account kwa elfu 10 tu.
Tafuta kibarua ambacho kwa siku hutakosa elfu 5 ya kuweka kwenye kibubu.
Unaweza menya viazi kwa wapika chips, osha magari, piga debe n.k
Baada ya mwezi nenda na kibubu benk kama uliweka elfu 5 kwa siku utakuta 150,000=
Zitawekwa kwenye account yako.
Rudi na kibubu endelea na zoezi baada ya miezi 12 utakuwa na 1,800,000= bank
Nunua maguta matatu au bodaboda moja, hesabu ya guta kwa dsm ni 5,000= anapolichukua asubuhi
na sio jioni anaporudi.
Endelea kumenya chipsi au kuosha magari sasa utaweka elfu 5 yako na 15,000= ya maguta, jumla kwa siku elfu 20, kwa mwezi laki 6 kwa miezi 12 utakuwa na 7,200,000= benk.
Mwaka wa tatu nunua bajaji, hesabu elfu 20.
Sasa kwenye kibubu utaweka elfu 5 yako, elfu 15 ya maguta na elfu 20 ya bajaji, jumla kwa siku utaweka elfu
40 kwa mwezi utakuwa na 1,200,000= kwenye kibubu, kipeleke benk, baada ya miezi 12 utakuwa na 14,400,000= Nunua bajaji 2 mwaka wa 4. jamani usiku mwema.
 
In which standard!? Do you wanna be a dollar millionaire or tanzania shilling millionaire?

Kama ni katika standard ya kitanzania hata ukitunza boom la semister mbili ukirudi kitaa wewe ni millionaire.
 
saving is important
 
Nisaidie hapo kwenye kibubu cha chuma mkuu
 
Waliulize mamilionea. Sasa humu wengi wafanyakazi, wanavyuo na wafanyabiashara ndogondogo ndo wakushauri ndugu? You must be kiding
The best way to learn anything is to consult an expert.
Asante sana mkuu umejibu vyema
 
Hapo ameanza na miaka mingapi?
ANAJITEGEMEA AU ANATEGEMEA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…