Tupeane uzoefu, hivi ni shughuli gani mtu ambae umeajiriwa unaweza ifanya kwa urahisi ukajiongezea kipato?

Tupeane uzoefu, hivi ni shughuli gani mtu ambae umeajiriwa unaweza ifanya kwa urahisi ukajiongezea kipato?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Habari wakuu , watumishi tulioajiriwa huwa tunatamani sana kujishughulisha ili mradi kipato kiongezeke lakini kwa ujumla huwa tunaface Changamoto zifuatazo zinazopelekea kushindwa :-

1. Tuna muda mchache wa kusimamia

2. Watu wengi sio waaminifu tunao waweka kwenye shughuli hizo

3. Tunaogopa sana ku take risk

Hivyo naomba tushare uzoefu mbali mbali

Binafsi nimewahi fanya bishara ya Vi body / vi blauzi vya kike nanunua 3000 Mwanza au Katoro nakuja kuviuza 7000 mpaka 12000.

Hii kwangu ilikuwa rahisi sababu nlikuwa najua nimechukua 200 au 300 hivyo nitegemee kiasi fulani na ninashukuru Mungu vilikuwa vinatoka mpaka nilipo badili mazingira .

Je, shughuli zipi nyingine ni rahisi?​
 
Habari wakuu , watumishi tulioajiriwa huwa tunatamani sana kujishughulisha ili mradi kipato kiongezeke lakini kwa ujumla huwa tunaface Changamoto zifuatazo zinazopelekea kushindwa...​
Nunua mazao weka ndani sali bei ipande uza, kama hauna muda wa kufatilia biashara kazi kama hii inakufaa japo unazika pesa lakin faida utaiona wakat wa kuuza ukifika
 
Habari wakuu , watumishi tulioajiriwa huwa tunatamani sana kujishughulisha ili mradi kipato kiongezeke lakini kwa ujumla huwa tunaface Changamoto zifuatazo zinazopelekea kushindwa...​
Tafuta eneo, piga nyumba za kupangisha kuwalenga low & medium class.
 
1. Tafuta sehemu nzuri uanzishe biashara ya miamana ya fedha.
2. Eneo zuri kulikochangamka kwa biashara ya chips
3. Eneo changamshi anzisha duka la vipodozi.
 
1. Tafuta sehemu nzuri uanzishe biashara ya miamana ya fedha.
2. Eneo zuri kulikochangamka kwa biashara ya chips
3. Eneo changamshi anzisha duka la vipodozi.
Hebu mpe mbinu ya kuepuka hizi challenge za hizi biashara?

1. Tuna muda mchache wa kusimamia
2. Watu wengi sio waaminifu tunao waweka kwenye shughuli hizo

#YNWA
 
Back
Top Bottom