Tupeni hela zetu tukafie mbele

Tupeni hela zetu tukafie mbele

Mtanzania2020

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
817
Reaction score
1,752
Inasikitisha wastaafu kutoa kauli kama hizi
1000419754.jpg
 
Inahuzunisha sana! Mtu unafanya kazi kwa nguvu zote unachelewa kulala unawahi kuamka halafu mwisho wa siku mafao yako utumie tena nguvu kuyaomba
Viongozi wanasababisha laana kwenye vizazi vyao.

Jasho la mtu haliendi bure..!
 
Mimi tangia kipindi kile nafuatilia Hela za Nssf ndo nilikuja kuona ni dhuluma na upuuzi sana! Pesa yako lakini kuna masharti kibao ya kuzitoa.

Nadhani wastaafu wengi wameacha mamilioni yao ni usumbufu..mtu kashafikisha 55 yrs sijui 60 mpe mzigo wake wote akafie mbele. Wengine maskini wanaugua magonjwa mbali mbali uwezo wa kufatilia hana...yaani daah

Mtu anajisifu NSSF yangu nina 20m sijui 30m e.t.c kuja kuipata hiyo ni kizungumkuti.
Naheshimu sana wafanyabiashara waliojiwekeza huu upuuzi sio kabisa.

Hii ilinipa funzo la kujiajili.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuchukua/kung'ang'ania haki ya mtu hii laana itawatafuna hata kama sio kwenye maisha haya yajayo Mungu atawaadhibu vibaya sana.Hii nchi sijui tuna tatizo gani jmn aaah!
 
Inahuzunisha sana! Mtu unafanya kazi kwa nguvu zote unachelewa kulala unawahi kuamka halafu mwisho wa siku mafao yako utumie tena nguvu kuyaomba
Viongozi wanasababisha laana kwenye vizazi vyao.

Jasho la mtu haliendi bure..!
Kuna uzi nimeona mtu anaejiita Lucas Mwashambwa anakutafuta.
 
Mtwara wamevurugwa. Nizaidi ya wadudu wa chuga
Kumbe umewaona wale wadudu,mi nimeguswa na yule wa mataili ya boda boda ila yamemtosha miguuni,
full burudani,unawahi mjini bila kutumia mafuta. ah ah ah ah
 
Inasikitisha wastaafu kutoa kauli kama hizi
View attachment 2978192
Nimeangalia maandamano,hili bango sijaliona,nimekerwa sana na kwaya ya watumishi wa umma
ila nimeipenda ile kwaya ya bandari angalau walikuwa 50/50.
Kimsingi sherehe za siku ya mfanyakazi hazikutakiwa kuwa za kisiasa, tulitarajia viongozi wawaalike viongozi wakuu
wa ILO n.k ila dah,mpaka uvccm walikuwemo kwenye maandamano sijui wanafanya kazi wapi?
 
Tulieni pesa zenu tunazitumia kununua V8 na kuwatunza wake wa viongozi wenu wastaafu pamoja na kulipa wabunge
 
Back
Top Bottom