Dadakidoti
JF-Expert Member
- Jul 26, 2024
- 399
- 1,409
Mmenikumbusha mbali enzi za heka heka za ujana nikaenda kwa x wangu nikakuta amenunua ricecooker sasa dada wa watu nilikuwa sijawahi hata kuiona. bwana yule akawa sebuleni kwake yuko bize na mambo yake nimewasha jiko la gesi nimepika mboga tena zaidi ya moja zimeiva lakini mchele hupo kwenye rice cooker unaniangalia kila nikifunua naona hupo vile no kuchemka no kufanya chochote. nami naona aibu kumwambia jamaa kama hii kitu sijui kuitumia naenda namchungulia narudi jikoni sijui cha kufanya mpaka nilipopata akili ya kumpigia videocall shoga yangu mmoja ndo nikatoboa sitokaa nisahau๐๐