Tupia changamoto yako uliyokutana nayo wakati wa kujifunza gari, pikipiki na vyombo vingine vya moto

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2019
Posts
13,284
Reaction score
24,047
Kama kuna changamoto yeyote uliyokutananayo wakati unaanza kujifunza chombo cha moto gari, pikipiki tupia hapa, naanza mimi.

Ilikuwa ni kwenye kota za NDC Mitaa ya Masaki, kwenye kota huwa kuna vibarabara. Sasa hivyo vinjia ndiyo nilikuwa nazunguka na gari kwa ajili ya kujifunza.

Siku moja nikapata mawazo ya kutoka nalo nje ya geti, bwana wee, ile nakaribia geti la kutokea nikakutana na toroli la taka, jamaa mwenye toroli kaniachia nafasi ndogo ya kupishana.

Nikapagawa badala ya kukanyaga break kupunguza mwendo nikakanyaga pedal ya mafuta, nikaburuza lile torori mpaka nje ya geti, ghafla gari ikazima mchezo ukaishia hapo.

Je wewe ulikutana na kasheshe gani?
 
Mimi siku ya kwanza kushuka k9 ilikuwa saa tisa usiku na sikuwa mwenyeji wa njia ile naona chuma inashuka tu mh nikaona hapa sasa nikisema niisikilizie hii chuma itaenda kunitupa mbele, kweli ktk harakati za kung'oa mihogo namaliza tu mbele kuna kona alafu kuna bonge la kicheche upande wangu. Nashukuru mungu nilikuwa nashuka na stopper hivyo nilipokanyaga kubwa chuma ikasimama. Sitoisahau hiyo siku sababu najua kama kutoka labda viatu tu.
 
haa kaka unashuka k9 usiku alafu njia huifahamu ni hatari sana,
unabahati trela lingekufunika kwenye horse

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kei naini ya ngara-kasharazi mkuu hilo ni eneo la machinjio. haikati mwezi lori halijabeba roho.

karibu tena ngara
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…