NAWATAFUNA
JF-Expert Member
- Nov 14, 2019
- 13,284
- 24,047
Kama kuna changamoto yeyote uliyokutananayo wakati unaanza kujifunza chombo cha moto gari, pikipiki tupia hapa, naanza mimi.
Ilikuwa ni kwenye kota za NDC Mitaa ya Masaki, kwenye kota huwa kuna vibarabara. Sasa hivyo vinjia ndiyo nilikuwa nazunguka na gari kwa ajili ya kujifunza.
Siku moja nikapata mawazo ya kutoka nalo nje ya geti, bwana wee, ile nakaribia geti la kutokea nikakutana na toroli la taka, jamaa mwenye toroli kaniachia nafasi ndogo ya kupishana.
Nikapagawa badala ya kukanyaga break kupunguza mwendo nikakanyaga pedal ya mafuta, nikaburuza lile torori mpaka nje ya geti, ghafla gari ikazima mchezo ukaishia hapo.
Je wewe ulikutana na kasheshe gani?