Tupia jina la memba mmoja wa JF ambaye katoweka humu

Mkuu Mdogo wako wamempiga ban!!
Msalimu sana
 
Mkuu Mdogo wako wamempiga ban!!
Msalimu sana
Yule kisirani chake anakijua mwenyewe.

Dakika moja anaongelea usomi na kuhubiri upole kama mtawa wa ki Buddha (alisoma sana temple, kisha akaipotezea akaenda kujichanganya Wall St), dakika nyingine, akishaona umemvunjia heshima tu, anakufurumushia matusi ya kichaa kumshinda 2Pac mpaka unashangaa kama huyu ni mtu yule yule au tofauti.

Anasema hapa wajinga wengi na bora hata hivyo anavyopigwa ban, maana akiwepo sana ataishia kutukanana nao tu, kitu ambacho kinaweza kuwa si kizuri kwa wasiostahili kuona uchafuzi wa jukwaa.

Yupo New Orleans sasa na bibie wake wameenda ku party Fat Tuesday ya Mardi Graas.
 
Mdomo wa bata nae kapotea sijui yu wapi
 
Nimemsahau yule aliyekukuwa anatupa mambo ya Mr 900 inapendeza manake yeye mpaka urusi alifika. Nani nisaidieni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…