Tupia makosa ya kiufundi ya kwenye movie

Tupia makosa ya kiufundi ya kwenye movie

olele

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
1,305
Reaction score
1,572
Mimi ni mpenzi sana wa movie, hasa za action na animation, siku za hivi karibuni nimejikuta nikipenda kuangalia makosa yanayofanywa na kuachwa bila kuondolewa wakati wa kufanya editing, sasa sijui ni makusudi au ni bahati mbaya hayo makosa yanaachwa hadi tunayaona kwenye movie (Maana najua hadi muvi itolewe inapitiwa kwenye mikono ya watu wengi kwa ajili ya kuhakikiwa.

Hii thread ni maalumu kwa ajili ya makosa kama hayo.

Naanza:

Kwenye movie mpya ya 6 Underground kuna mahali mwanzoni kabisa walikua wanafukuzana magari, gari ya kijani iliyowabeba "Masterings ilikoswa koswa kugongwa na lorry lakini ikang'o site Mirror ya upande wa kushoto kama inavyoonekana hapo

capture .JPG

Lakini baada ya muda mfupi sana (baada ya tukio tu la kugongwa) hiyo gari ikaonekana iko na site mirror zote mbili

Capture 2.JPG

Ina maana hadi movie inatoka hakuna mtu yeyote aliyegundua hilo kosa na ni uzembe wa nani, kati ya Editor, Director nk.

Karibuni wadau
 
Kuna movie kacheza The Rock, nadhani ni Fast and Furious. The Rock alishika kamba ambayo inavyutwa na helicopter akiwa kwenye gari na aliishinda nguvu helicopter[emoji23]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom